Tangazo

March 28, 2013

Rais Dk. Kikwete azindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria vya Ukimwi na Malaria Mwaka 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata ukanda kuzindua rasmi taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Mhe William Lukuvi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akinyanyua juu baada ya  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda',  Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipitia baada ya kuzindua rasmi  taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012 leo Machi 27, 2013 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda na kushoto kwake ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi, Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa.

 Wadau kutoka sekta mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.

Meza kuu ikimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiri Ukimwi (TACAIDS) Mama Fatma Mrisho akisoma taarifa ya utafiti wa viashiria vya ukimwi na malaria mwaka 2012. PICHA NA IKULU

No comments: