Tangazo

May 21, 2013

JK AONGOZA KIKAO CHA CC YA CCM MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe, wakati wa Kikao Cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, kilichofanyika leo May 21, 2013, kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Bashir Nkoromo)

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kufungua kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM, leo Mei 21, 2013,  kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, wakiwa mkutano wa Kamati hiyo, leo Mei 21, 2013,  kwenye ukumbi wa Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

No comments: