Tangazo

July 9, 2013

Airtel Rising Star 2013: Mwanza wanaume na Kinondoni wasichana waibuka kidedea

Wachezaji sita nyota ( waliokaa) waliochaguliwa kuhuduria Clinic itakayoongozwa na makocha wa kabla ya Manchester united wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa katika final za Airtel Rising stars zilizofanyika katika katika viwanja vya karume jijini Dar es Saalam.

 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akikabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars kwa nahaodha wa timu ya Mwanza Kelvin Faru kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki.

 Timu ya Mwanza ikifurahia  ushindi  mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za Airtel Rising Stars kwa mwaka 2013.
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam.

 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos, akifatiwa na Raisi wa TFF sir Leodgar Tenga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso wakikangua timu kabla ya kucheza mechi ya finali katika michuano ya Airtel Rising Stars , mechi ilikuwa kati ya Morogoro na Mwanza.

 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos akiongea na wachezaji kabla ya kuanza mechi za fainali.
 Mlinzi wa Mwanza Ally Mnasi (kushoto) akipambana na Evance Robert wa Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki.   Mwanza walishinda 1-0.

 Rais wa TFF Leodegar Tenga akimvisha medali kocha wa timu ya taifa ya vijana Jacob Michaelsin kutambua mchango wake kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yaliyomalizika uwanja wa Karume mwishoni mwa wiki

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Levi Nyakundi akikabidhi mfano wa hundi kwa  mchezaji bora wa Airtel Rising Stars  Anna Hebron kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments: