Tangazo

July 31, 2013

BENKI YA NBC YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto), akiwa na Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji NBC, Mizinga Melu katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibar jana.

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (kulia), akichukua futari katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mjini Zanzibar jana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Kushoto ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  wa Zanzibar, Zahra Ali Hamadi (kulia), Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Mwanaidi Saleh  Abdallah (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) wakichukua mlo wa futari iliyondaliwa na benki hiyo mjini Zanzibar jana.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na NBC Kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Katikati ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.

Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Khamis baada ya hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao mjini Zanzibar jana. Nyuma ya Dk Kassim ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Mizinga Melu.

Baadhi ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Kisiwani Zanzibar jana.

No comments: