Tangazo

August 15, 2013

Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015: UNESCO na UNDP zaendelea kuzipiga msasa Redio za Jamii ili kutekeleza Mradi wa Demokrasia na Amani

IMG_2404
Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akitoa mada kwa wadau wakati wa warsha ya Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii kuhusiana na umuhimu wa kutengeneza vipindi vyenye ubora vitakavyovutia jamii wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza ambayo imefadhiliwa na UNDP na kuratibiwa na UNESCO.
IMG_2285
Mwezeshaji kutoka Search for Common Grounds Patricia Loreskar akizungumza na Mameneja wa redio za jamii nchini kuhusiana na shirikika lake linavyofanya kazi ya kutoa Elimu kujenga Amani na kutatua migogoro mbalimbali inayojitokeza kwenye jamii yetu na kuwataka redio za jamii zisiwe chanzo cha kuvuruga Amani bali zitoe Elimu ya kudumisha Amani kwa jamii nchini kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM kwa redio za jamii nchini kwa ajili ya kujiandaa kuendesha mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
IMG_2393
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin akifafanua jambo wakati wa warsha ya wiki moja ya Majadiliano baina ya Vyombo vya habari vya kijamii (redio) na nafasi yake katika kuhamasisha Demokrasia na Amani kwenye mazingira shirikishi na umuhimu wake katika kuunganisha jamii na kutatua migogoro ikiwa ni moja ya jitihada za kuendeleza Elimu haswa katika kuboresha sera za uhariri wa habari.
IMG_2306
Picha juu na chini ni Baadhi ya Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii wakifuatilia mada mbambali zilizokuwa zikitolewa kwenye Warsha ya wiki moja inayoendelea katika kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza.
IMG_2121
IMG_2331
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Grace Mapunda akizungumzia uhusiano wao na redio ya jamii Sengerema FM ambao amesema redio hiyo imekuwa mchango mkubwa sana kwa wananchi wa wilaya hiyo katika kupashana habari.
IMG_2424
Meneja wa Redio Jamii ya Orkonerei Fm ya Wilayani Simanjiro Khadija Abdallah akiwasilisha mada kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.
IMG_2102
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mtafiti kutoka ECOM Research Dr. Ambrose Kessy akielezea umuhimu wa kufanya utafiti kwa redio za jamii kwa ajili ya kuboresha usikivu na vipindi vyao kwa jamii.
IMG_2346
Meneja wa Kituo cha redio ya Jamii FADECO Adeline Lweramula akichangia maoni yake wakati wa kujadili uboreshaji wa sera za uhariri wa habari. Kulia ni mwezeshaji Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO Yusuph Al-Amin.
IMG_2323
Meneja wa mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins (kushoto) akibadilishana mawazo na wadau wa Search for Common Grounds wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema FM mkoani Mwanza.

No comments: