Muonekano wa nje wa Hoteli ya LISBON wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza lilipotokea tukio la wizi wa mali za mteja.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Na Mwandishi wetu
Katika hali isiyo ya kawaida Meneja Mawasiliano wa Pangani FM Bw. Abdallah Mfuruki ameibiwa dola mia moja za Kimarekani, vitambulisho vya kazi na lesse ya kuendeshea gari pamoja na shilingi laki moja na nusu za Tanzania katika mazingira ya kutatanisha.
Tukio hilo limefanyika usiku wa manane akiwa amelala ndani ya Hoteli ya LIZIBON iliyoko wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Bw. Mfuruki amesema kuwa aliibiwa vitu hivyo Agosti 15 mwaka huu ndani ya hoteli hiyo aliyofikia mjini humo kuhudhuria mafunzo ya redio za jamii kuhusu demokrasia na amani katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na UNESCO pamoja na UNDP yanashirikisha maneja 25 wa redio za jamii nchini.
Amesema baada ya kuibiwa alitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini Sengerema na kupewa RB Namba SEN /M/146.
Baada ya kufika katika eneo la tukio na polisi kujionea hali halisi ya tukio hilo, Mmoja wa Askari waliofika kushuhudia tukio hilo alikiri kuwa hoteli hiyo imekumbwa na matukio hayo mara kwa mara akiwemo yeye kuibiwa siku za karibuni akiwa amelala hotelini hapo.
Amesema suala hilo linahitaji ushirikiano wa karibu ili kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kwa upande wake Meneja wa Hoteli hiyo Bw. Sosipita Shadrak alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuonesha kushangazwa na tukio hilo wakati akijua wazi chumba namba 207 alichompatia mteja wake dirisha lake lilikuwa bovu kwa muda mrefu.
Kitendo hicho kimewasononesha mameneja wengine waliohudhuria mafunzo hayo na kuiomba mamlaka husika kufanya jitihada za haraka ili sheria ichukue mkondo wake na vitu hivyo vilivyoibiwa vipatikane kwa wakati muafaka.
Wamesema pia kuwa iwapo sheria haitatendeka iko haja kuandika au kutoa tamko ambalo linaweza kuharibu jina la hoteli au wilaya ya Sengerema kwa ujumla.
Wanahabari tunajiuliza ndio tuseme utawala wa hoteli ya LIZBON unashirikiana na wezi au wenyewe ndio wanaoiba vifaa vya wateja? Kwa sababu kwa nini wasichukue hatua ya kutengeneza dirisha hilo lililoharibika muda mrefu la chumba namba 207 ambako kila wakati kunatokea matukio ya wizi?
Tunatumaini polisi watafanya kazi yao na mali za mwenzetu ziweze kupatikana na hatua zitachukuliwa kwa hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment