Tangazo

August 6, 2013

Mhasibu aibuka mshindi wa Nyumba kupitia promosheni ya 'Airtel Yatosha'

Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando  akiongea wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza kupitia promosheni ya Airtel yatosha , kushoto Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao kulia Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel yatosha ilimpata mshindi wa nyumba bwana Silvanus Juma kutoka mkoa wa iringa

Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando , Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao kulia Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakisubiri draw ya kutafuta mshindi itafute namba ya mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza kupitia promosheni ya Airtel yatosha.

Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia akiongea na mshindi wa nyumba mara baada  ya kupatikana katika draw ya mwenzi iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo bwana
Silvanus Juma kutoka mkoa wa iringa aliibuka mshindi wa nyumba hiyo wakishuhudia Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao katikati akifatiwa na Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando
*******************************
Airtel Tanzania Agosti 05, 2013 imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba  kupitia promosheni ya Airtel yatosha Shinda nyumba inayoendelea  na kuwazawadia wateja wake kila siku ambapo Bw. Silvanus Juma mkazi wa Iringa (33) ambaye ni Mhasibu wa shirila la Tanzania Rural Women and Children Development Foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa  nyumba ya kisasa iliyojengwa na Shirika na Nyumba la Taifa (NHC) iliyopo Kigamboni jijini Dar es saalam.  

Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando alisema" kama tulivyowangazia awali leo ndio ile siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba  na tumeshuhudia bwana Silvanus Juma  akiibuka mshindi kupitia droo ya kwanza tuliyoichezesha hapa.

Sambamba na hilo leo tunao washindi 7 wa wiki  kutoka katika mikoa mbalimbali ambao hawa wataondoka na pesa taslimu shilingi  milioni moja kila moja, washindi hawa ni pamoja na  Peter Ignasho kutoka Muheza Tanga, Edita Rweyabura  kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh Ali Mauji, Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo kutoka Manyoni Singida and Vero Mispela Kiwango kutoka Bihalamulo.

Alitoa wito kwa watanzania na wateja wetu kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi mbalimbali na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali , kujiunga nirahisi piga  *149*99#
kisha nunua kifurushi chacko cha  siku, wiki au mwezi  na kisha kuingizwa moja kwamoja kweny droo ya kuweza kushinda milioni moja kila siku au zawadi kubwa ya Nyumba.

Akiongea kwa njia ya simu baada ya kutangazwa mshindi Bw. Silvanus Juma alisema"Ninayofuraha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel napenda kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel waendelee kutumia huduma ya Airtel yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo.

"Binafsi sijawahi kushinda Bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba ushindi ni wa uhakika usio na upendeleo wala ubaguzi hivyo wajaribu nao wanaweza kuwa washindi", alisema Bw. Juma.

Kwa upande wake moja ya wafanyakazi wenzake Bw. Beatus Magoti ambaye ni Mshauri wa fedha na tawala TARWOC alisema"  tumefurahi sana kuona kijana mgodo mwenzetu ambaye ni mchapa kazi ameweza kushinda nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha. Hii imetupa hamasa na sisi kushiriki na kueneza habari kwa wengine kushiriki na kushinda kama laivyoshinda Silvano.

Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel yatosha. 

Sambamba na hilo Airtel pia imewawezesha wateja wake nchi nzima  kutuma na kutoa pesa bure bila makato yoyote.

No comments: