Tangazo

August 23, 2013

UNIC YAWATAKA VIJANA KUJITAMBUA MAPEMA ILI KUJENGA TAIFA LITAKALOKUWA NA VIONGOZI WENYE MTIZAMO CHANYA

IMG_3438
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyampulukano ya Wilayani Sengerema Mwl. Vedastus Mlokozi wakati alipofika shuleni hapo kuwahamisha wanafunzi kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa.
IMG_3441
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akisaini kitabu cha wageni shuleni hapo.
IMG_3480
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyampulukano ya Wilayani Sengerema mkoani Mwanza wakati alipotembelea shuleni hapo kuhamasisha Wanafunzi kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa.
IMG_3489
Mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyampulukano ya mjini Sengerema akiuliza maswali kwa Bi. Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
IMG_3526
Mwalimu wa Shule Sekondari Nyampulukano ya Wilayani Sengerema akizungumza jambo na Wanafunzi wake.
IMG_3558
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama aliyeambatana na mwenyeji wake Mkuu wa vipindi redio ya jamii Sengerema FM Bw. Andrew Mfungo wakizungumza na Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Sengerema Bw. Nelson Rwelengela (kulia) ofisini kwake mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
IMG_3563
Mlezi wa UN Club ya Sengerema Sekondari Mwl. John Kimbuli akielezea shughuli za UN Club shuleni hapo na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama alitembelea shule hiyo mwishoni mwa Juma.
IMG_3575
Makamu Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Sekondari Sengerema Bw. Nelson Rwelengela (aliyesimama meza kuu) akiutambulisha ugeni kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa Wanfunzi wa shule hiyo.
IMG_3629
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa Sengerema High School, kuhusiana na umuhimu wa kuanzisha vilabu vya Umoja wa Mataifa mashuleni, na kufafanua kuwa hiyo ni moja ya agenda za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa vijana zake ikiwamo Malengo ya Milenia (MDGs) kwa sababu kupitia wao wataweza kuzifahamu vizuri na mapema agenda mbalimbali za Umoja wa Mataifa wakiwa bado vijana, ili waweze kuzitekeleza hapo baadae.

Pia amewagusia suala la kujiepusha na marafiki wenye tabia mbaya itakayowapelekea kujihusisha na vitendo visivyo vya kimaadili ikiwemo uvutaji bangi na matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili Tanzania kwa sasa, aidha amewasaa kutojihusisha na ngono pindi wawapo mashuleni ili kujiepusha na gonjwa la Ukimwi.

Awali akizungumza na vijana wa shule za sekondari Nyampulukano wilayani Sengerema mkoani Mwanza Bi. Usia Nkhoma Ledama amewaeleza vijana upo umuhimu mkubwa sana kwa wao kujitambua, kwani kutawasaidia kupanga maisha yao kwa kuchagua nini unataka kufanya na njia gani ufanye ili uweze kufanikiwa.
IMG_3633
Bi.Usia amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu vya vijana vya Umoja wa Mataifa (UN Club) mashuleni, basi hawana budi kujiunga kwa wingi zaidi kwani kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kusaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.

Aidha amewatolea vijana hao mfano kuwa hata Waheshimiwa January Makamba (Mb) na John Mnyika(Mb) walikuwa wanachama wa vilabu hivyo ya vijana vya Umoja wa Mataifa wakati wakisoma shule za sekondari, kitu kilichowajengea uwezo na kujiamini na mpaka sasa wamekuwa viongozi wenye nafasi za juu hapa nchini, na kuwataka vijana kuiga mfano wao.
IMG_3679
Picha juu na chini Wanafunzi wa Sengerema Sekondari wakiuliza maswali kwa Bi. Usia Nkhoma Ledama.
IMG_3670
IMG_3689
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sengerema wakifura kupigwa picha walipotembelewa shuleni hapo na Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
IMG_3690
Bi. Usia Nkhoma Ledama akibadilishana mawazo na Wanachama wa UN CLUB Sengerema Sekondari pamoja na Mlezi wao.

No comments: