Mtoto mkazi wa Kunduchi, Rukia Ramadhani akipimwa uzito katika kliniki ya wamama na watoto iliyokuwa ikiendeshwa na wahudumu wa gari la kutolea huduma za afya linalotembea (Mobile Clinic) la Benki ya NBC mahali hapo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Gari hilo ni moja ya magari matano yaliyotolewa kwa Bodi ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam ili kutoa huduma za afya bure kwa wamama na watoto maeneo ya vijijini. Anayempimawa pili kulia ni muuguzi wa gari hilo, Eliza Shayo. |
No comments:
Post a Comment