DCP Mohamed Mpinga |
* Mwaka huu yadhamini tena
uchapishaji wa stika za usalama barabarani pamoja na wiki ya usalama barabarani
Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi nchini,
Airtel imetajwa kuwa moja kati ya makampuni ambayo amekuwa yakishirikiana na
serikali kwa dhati katika harakati za kupambana na tatizo la ajali za
barabarani.
Akithibitisha madai hayo, Kamanda mkuu wa
kikosi cha usalama barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga amesema kuwa Airtel
imeweza kutoa mchango katika kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi kikubwa ikitoa ushirikiano katika juhudi
mbalimbali zinazofanywa na kikosi cha usalama barabarani kwa dhumuni la
kuepusha ajali za barabarani.
"Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama
barabarani, kwa miaka mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel
inaendelea na udhamini wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Airtel pia
imedhamini vipindi vya elimu ya usalama barabarani katika TV - kumekucha na
Jambo Tanzania
(ITV na TBC 1) na Radio one.
Pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na
jeshi la polisi usalama barabarani imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao
Kuendesha + Simu = Kifo inayowaasa waendesha vyombo vya moto kutotumia simu
wakati wakiendesha magari, vile vile mwaka jana
Airtel ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (Bodaboda)
yaliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki
," alisema DCP Mpinga.
Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania
Bi Beatrice SinganoMallya, akizungumza juu ya suala hilo , amesema "Airtel imeamua kushirikiana
na serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi la ajali za barabarani. Idadi ya vifo
vinavyotokea barabarani ni kubwa mno na ndiyo maana Airtel imeamua
kujikita katika kuokoa maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujuma.
Tunapenda kuwakumbusha watanzania kuwa swala la kupunguza ajali za barabarani
ni wajibu wa kila mwananchi hivyo tutii sheria bila shuruti"
Airtel itaendelea kushirikiana na jeshi la
polisi usalama barabarani katika kuhakikisha lengo letu la upunguza ajali linafanikiwa, tumeanza kuona
mafanikio na kwa kiasi Fulani ajali za barabarani zinapungua kulinganisha na
miaka iliyopita," alisema Beatrice.
Tumepatiwa Takwimua kwa na ofisi inayoratibu
wiki ya nenda kwa usalama barabarani zinabainisha ajali za barabarani zimeweza
kupungua kwa kiasi kikubwa tokea mwaka 2011 ambapo Airtel imekuwa ikishirikiana
nao katika programu mbalimbali mjini na vijijini, kabla ya hapo tokea mwaka
1995 ajali zilikuwa zikiongezeka kila mwaka kati ya ajali 2,000 na 4,000. Lakini Mwaka 2010
ukilinganisha na 2011 ajali zilipungua kwa 3% na 2011 na 2012 ajali
zilipungua kwa 2%.
Airtel Tanzania inaendelea na kudhamini
wiki hii ambapo kwa mwaka huu imejitolea kuchapisha tena stika za usalama
barabarani pamoja na kudhamini tena mashindano ya mpira wa miguu ya waendesha
bodaboda yajulikanayo kama MPINGA CUP ambayo dhamira yake ni kuunga mkono juhudi
za baraza linaloshughulikia usalama barabarani maalum kwa kutoa elimu kwa
watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu barabara zote ili kuepusha ajali.
No comments:
Post a Comment