Tangazo

September 24, 2013

Athuman Hamis Balozi wa Usalama Barabarani

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel katika wiki  ya usalama barabarani, mwandishi huyu alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel Tanzania ambao wamekuwa wadhamini wakuu wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa mwaka wa tano mfululizo Bi. Beatrice Singano Mallya akisalimiana na  Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel katika wiki hii ya usalama barabarani mkoani mwanza. Athumani alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini.
Airtel yahimiza Usalama Barabarani uzingatiwe.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Simu ya Airtel imesema kuwa itahakikisha suala la Usalama barabarani linazingatiwa na jamii ya Watanzania ili kupunguza ajali za barabarani .

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel,Beatrice Mallya kwenye ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya UsalamaBarabarani,yanayofanyika Jijini Mwanza.

Alisema kama wadau wa usalama barabarani,wamedhamini maadhimisho hayoili kuwezesha jamii kupata elimu na uelewa kuhusu matumizi yabarabara,sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani katika kupunguza ajali nchini.

alisema ajali nyingi nchini zinachelewesha maendeleo na kupunguza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Sisi kama wadau tumedhamini maadhimisho haya kwa mwaka wa tano mfululizo,lengo letu tunataka jamii ipate uelewa na hatimaye kupunguza ajali za barabarani zinaoweza kuepukika,ndiyo sababu tuko hapa,”alisema.

Alisema kutokana na kuonesha umahiri wameanzisha mfumo mpya wa ulipiaji  wa leseni za magari kwa kupitia  njia ya Airtel Money.

No comments: