Baadhi ya vijana wanaodai kuwa wanatoka mkoa wa Kigoma wakiwa wajaza fomu leo ambao taarifa zao zinaendelea kuchunguzwa kama kweli ni Watanzania wakiwa katika Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dares Salaam. |
Gari la Idara ya Uhamiaji likiwa limebeba baadhi ya watuhumiwa hao mara baada ya kutoka mahakamani. |
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
OFISI ya Uhamiaji mkoa wa Dares Salaam imemfikisha mahakamani Mtanzania anayedaiwa kuwatunza raia watano kutoka Nigeria wanaoishi nchini bila kibali halali baada ya kuwapiga na kuwazuia kufanya kazi maofisa wa uhamiaji kwenye ofisi za Serikali.
Hayo yalisemwa leo na Ofisa wa Uhamiaji wa Mkoa wa Dares Salaam, Grace Hokororo wakati akizungumza na mwandishi wa Idara ya Habari –MAELEZO ofisini kwake ambapo alisema Mtanzania huyo alifikishwa leo(jana) katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu baada ya kutenda kosa hilo jana majira ya saa 1:00 jioni.
Alimtaja Mtanzania huyo kuwa ni Christopher Kanyala mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati miaka 29 hadi 34 mkazi wa Sinza na anadaiwa kuwa aliwaHI kutumikia Jeshi la Polisi nchini, ambapo kesi yake na raia hao watano wa Nigeria itatajwa kesho katika mahakama hiyo.
Akizungumzia kuhusu suala hilo , Grace aliwataka wananchi wasipende kuishi na raia ambao ni wageni na hawajaripoti katika ofisi za uhamiaji kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria. Huku akiwataka raia wa kigeni kuripoti katika ofisi hizo mara baada ya kuwasili nchini ili waweze kufuata taratibu za kisheria.
Aidha alisema operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu inaendelea vizuri.
Grace alisema kwa upande wa wahamiaji haramu kutoka Malawi walijitokeza kwa hiari mpaka leo mchana idadi yao imefikia 1,863 tangu zoezi hilo lilipoanza.
Aliongeza kuwa opresheni hiyo imehusisha mataifa 31 ambapo alitaja baadhi yake kuwa ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda,Italia, Singapore Ethiopia,Libya Yemeni,Somalia,Komoro, Ujerumani, Afrika Kusini,Uturuki, Nigeria, Cameroon,Liberia na Bokinafaso., Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo(DRC) na India.
Alisema jumla ya raia hao wa mataifa mengine waliokamatwa ni 502.

No comments:
Post a Comment