Na Eleuteri Mangi- Maelezo
SERIKALI
ya Tanzania
na Uswisi zimetiliana mkataba makubaliano wa kuisaidia mpango wa taifa wa kupambana na malaria nchini
(NMCP) nchini wenye thamani ya Sh. bilioni 10.3.
Mkataba
huo wa makubaliano hayo umetiwa saini leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Uchumi Dkt. Servancius Likwalile na Balozi wa Uswisi nchini
Olivier Chave.
“Nimefurahi
kubainisha kuwa lengo kuu la kutia saini makubaliano ya msaada huu ni kupunguza
vifo vya watoto na akinamama vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria hasa
makundi hayo hatarishi kwa kuimarisha na kusaidia NMCP,” alisema Dkt. Likwalile.
Dkt.
Likwalile alisema kuwa Serikali ya Tanzania inaichukulia Serikali ya
Uswisi kuwa ni moja kati ya rafiki waaminifu katika masuala ya maendeleo.
Alisema
kwa takwimu za hivi karibuni, matokeo yanaonesha kuwa kumekuwa na maboresho
mazuri hasa katika kuzuia malaria kwa watoto chini ya umri wa miezi sita hadi
59 vimepungua zaidi ya nusu kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi asilimia 10
mwaka 2012.
Aidha
Dkt. Likwalile alisema kuwa kumekuwa na maendeleo mazuri ya kupambana na
ugonjwa wa malaria licha ya changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya afya.
Changamoto hizo ni pamoja na ukweli
kwamba kwa upande wa Tanzania Bara, ugonjwa wa malaria bado ni tatizo kubwa
linalowasumbaua Watanzania walio wengi ambapo zaidi ya asilimia 93 bado
wanaishi katika mazingira hatarishi ya uwezekanao wa kuambukizwa ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa madhara yanayotokana
na ugonjwa huo yanaiathiri jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu
ambapo wanafunzi hushindwa kumudu masomo hasa wanapokuwa.wagonjwa.
Pia wafanyakazi na wakulima wanapougua
hushindwa kutekeleza majukumu yao .
Hivyo kupelekea familia na jamii kushindwa kuendesha maisha yao ya kila siku.
Kwa upande wake Balozi wa Chave alisema
kuwa matokeo yanaonesha Tanzania
inafanya vizuri katika kupunguza ugonjwa wa malaria ambapo takribani asilimia 91 ya wakazi wanatumia vyandarua, asilimia 72 ya watoto chini ya
miaka mitano na asilimia 74 ya wanawake wajawazito hulala katika vyandarua
vilivyowekwa dawa ya kuzuia mbu.
“Lengo la mradi ni kusaidia NMCP katika kuzuia kuudhibiti na kutibu
ugonjwa wa malaria hasa katika kusimamia, kupima na kutoa dawa za malaria kwa
ufanisi mkubwa,” alisema Chave.
Balozi Chave alisema kuwa mradi huo
unaofadhiliwa na nchi yake umekuwa na mafanikio makubwa ambapo takribani
asilimia 48 ya vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano vimepungua kati
ya mwaka 2000 hadi 2010.
Kwa mantiki hiyo Balozi Chave alisema
kuwa Tanzania
inaweza kufikia malengo ya millennia namba nne ifikapo 2015 ambapo ni nchi
chache za Afrika zinaweza kufikia malengo hayo.
Naye Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando
alithibitisha kuwa wizara yake itasimamia fedha hizo kulingana na malengo
yaliyokusudiwa.
Ushirikiano huo wa maendeleo
baina ya nchi hizo ulianza kati ya miaka ya 1960 uliolenga katika kudhibiti
malaria wilaya ya Ifakara mkoa wa Morogoro na mwaka 1981 serikali hiyo kupitia
Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) lilijikita katika utoaji huduma za afya
kwa lengo la kuendeleza upatikanaji wa huduma bora za kiafya maeneo
ya vijijini.
No comments:
Post a Comment