Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji pamoja na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili Oktoba 28, 2009 baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV na kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake wote kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo. |
No comments:
Post a Comment