Tangazo

January 29, 2014

KUELEKEA KILELE CHA MIAKA 37:CCM YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mkutano wa CCM Mkoa wa Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano katika ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
######################################

   Wakati CCM inatimiza miaka 37 tangia kuanzishwa kwake februari 5 mwaka 1977,Chama hicho kinajivunia sana mafanikio makubwa kiliyopata hasa katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwa  Watanzania ,kutunza na kuilinda Amani ya nchi hii na kujenga misingi imara ya uchumi wa nchi,akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa wa Mbeya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  alisema  sherehe za miaka 37 zimeanza nchi nzima na zilizinduliwa rasmi tarehe 26 na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein Unguja Zanzibar.

  Kilele cha sherehe hizi  kitakua tarehe 2 februari ,Nape alisema “kwa nini tarehe mbili na sio tano ni kwa sababu tarehe tano ni siku ya kazi hivyo tumeona tufanye tarehe mbili ili tuwaruhusu watu wengi zaidi waweze kushiriki”
Sherehe hizi zitahitimishwa hapa jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine na zitahitimishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
Viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa CCM wameanza kuwasili na kesho anategemewa kuwasili Makamu Mwenyekiti  wa CCM (Bara) Ndugu Philip Japhet  Mangula ambaye pia ni mlezi wa mkoa wa Mbeya  akitanguliwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Nape alisema “Tarehe 2 asubuhi saa moja kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama ,Rais Jakaya mrisho Kikwete matembezi hayo yatafanyika kwenye jiji la Mbeya yataanzia eneo la Soweto na yataishia kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mbeya, baada ya matembezi hayo wananchi watakwenda kwenye viwanja vya Sokoine ambapo kutakuwa na burudani mbali mbali vikiongozwa na TOT, Vikundi vya muziki wa kizazi kipya, sherehe hizo zitaonyeshwa moja kwa moja na baadhi ya televisheni pamoja na kurushwa moja kwa moja na baadhi ya radio.
Wakazi wa Mbeya waombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi  tarehe moja na pia washiriki kwenye matembezi na sherehe zitakazofanyika tarehe2.

Maadhimisho ya sherehe hizi yataambatana na shughuli mbali mbali nchi kote ,ikiwa pamoja na shughuli  za utunzaji wa mazingira kama kupanda miti,kushiriki shughuli za maendeleo kujenga shule na zahanati,usafi  pamoja na kutembelea wagonjwa hospitalini.

No comments: