Tangazo

April 18, 2014

RAIS KIKWETE NA WANAFUNZI KATIKA PANTONI, AHANI KIFO CHA KADA WA CCM, APOKEA TUZO ALIYOTUNUKIWA MAREKANI

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe wakiongea na watoto Samir Juma (fulana nyekundu) na Salum Chumu wakiwa katika pantoni la MV Magogoni wakivuka kuelekea Kigamboni jijini Dar es salaam April 17, 2014. Watoto hao ambao wanasoma darasa la  awali katika shule ya msingi ya Bunge, walipata bahati ya kuketi na viongozi hao waliokuwa wakielekea kuhani msiba wa kada wa CCM Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuhani na kutoa heshima za mwisho kwenye msiba wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam April 17, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa  heshima za mwisho kwa mwili wa kada wa CCM na mwenyekiti wa Washirika kitaifa mstaafu Marehemu Edward Masanja Ng'hwani maeneo ya Kibada jijini Dar es salaam April 17, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakiangalia cheti cha heshima alichopewa na Gavana wa Maryland wakati wa kupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kupokea toka kwa  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membekupokea Tuzo ya Uongozi Bora Afrika aliyotuzwa nchini Marekani ambako aliwakilishwa na Mhe Membe. PICHA NA IKULU
RAIS JAKAYA KIKWETE APOKEA TUZO YA KIONGOZI BORA BARANI AFRIKA.
 
Na. Aron Msigwa- MAELEZO.
Dar es salaam.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam amepokea Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika kufuatia mchango mkubwa alioutoa  kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania na Bara la Afrika.
 
Akiwa mwenye furaha mara baada ya kupokea tuzo hiyo ambayo awali ilipokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe jijini Washngton Marekani,  Rais Kikwete amesema kuwa ameipokea tuzo hiyo kwa moyo wa shukrani na heshima kubwa kufuatia imani kubwa iliyoonyeshwa kwake na kwa watanzania.
 
“Nimeipokea tuzo hii kwa moyo wa ukunjufu, ni tuzo ya watanzania wote kwa sababu mambo yote niliyoyafanya sikuwa peke yangu nimeyafanya kwa kushirikiana na watanzania wote” Amesema Rais Kikwete.
 
Rais Kikwete amesema kuwa amepokea tuzo hiyo kufuatia wasomaji na wadau wa Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington kuonyesha imani juu yake kwa kumchagua kwa njia ya kura ya maoni kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika kwa mwaka 2013.
 
“Nawashukuru sana African Leadership Magazine, kwangu ni heshima kubwa nawaomba watanzania tuendelee kushirikiana wenzetu duniani wanaona, wanatambua na kuthamini mchango wetu” Amesisitiza Rais Kikwete.
 
Awali kabla ya kumkabidhi Rais Jakaya Kikwete Tuzo hiyo na cheti cha shukrani Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa tuzo hiyo ni heshima kwa taifa la Tanzania kufuatia juhudi kubwa alizoonyesha Rais Jakaya Kikwete katika kuboresha maisha ya watanzanzania.
 
Amesema  kuwa wasomaji na wadau wa jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine wamemuona Rais Kikwete kuwa Kiongozi Bora wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013 kwa kumpigia kura nyingi za maoni.
 
Aidha ameeleza kuwa Rais Kikwete alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo katika sherehe kubwa iliyotangazwa na kuonyeshwa moja kwa moja na mitandao mbali mbali ya kijamii duniani pia kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashuhuri wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Marekani na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugay ambaye alikuwa Washington kikazi.
 
Wengine ni Mwakilishi katika Bunge la Wawakilishi wa Jimbo la Georgia nchini Marekani na mwenyekiti wa wabunge weusi katika Bunge hilo, Bi. Dee Dawkins-Haigler na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
 
Rais Kikwete amepata tuzo hiyo akimfuatia Rais wa Sierra Leone , Mheshimiwa Ernest Bai Koroma, ambaye alishinda Tuzo hiyo mwaka 2012.

No comments: