Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi
Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti
Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika
Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
*****
Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni
jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali
na miundo mbinu mbalimbali .
Uharibifu mkubwa na wahatari ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme
kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.
Katika eneo la Mlalakuwa mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa
unaelekea kawe pana nguzo tatu ambapo
nguzo moja imevunjika kabisa na nyingine
mbili zimelegea katika nguzo iliyo
vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo
wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu
ya mti ulio pandwa pembeni mti huo si
mkavu ni mbichi.
Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme
wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo
mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu
wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?
Tunaomba muchukue
hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae kwani ni hatari sana
Picha na Dar es salaam yetu Blog
No comments:
Post a Comment