Tangazo

May 10, 2014

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO APOKEA NISHANI YA HESHIMA NCHINI NIGERIA

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa ofisini kwake huku akiwa amevaa nishani hiyo.

xxxxxxxxxxxxxxxxxx

Dar es Salaam

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mapema Machi mwaka huu  alikabidhiwa  nishani ya  kumbukumbu  ya Profesa M.O. Oyawoye aliyewahi kuwa  Profesa wa kwanza duniani kutoka Bara la Afrika katika masuala ya jiolojia  huko nchini Nigeria. 

Profesa Muhongo alikabidhiwa nishani hiyo na timu ya wanajiolojia  kwa kutambua mchango wake mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. 

Nishani hiyo alikabidhiwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay kwa niaba yake.
Habari & Picha kwa hisani ya Wizara ya Nishati na Madini

No comments: