xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Umoja wa wafanyakazi
wanawake wa Airtel ujulikanao kama Airtel Divas umejitoa kuwasaidia na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu
Tanzania (SWAUTA ) kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi hao wa Airtel walifanya
uzinduzi rasmi wa Airtel Divas na kualika kikundi cha SWAUTA kuonyesha na
kuuza bidhaa zao kwa wafanyakazi wa Airtel na kuwawezesha kupata fedha kwaajili
ya kuwa na banda lao katika maonyesho ya 38 ya kimataifa ya SABASABA.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja
Rasilimali watu Sophia Melamali alisema” tunayofuraha kuzindua rasmi Airtel
Divas mpango maalumu wenye lengo la kuwainua na kuwahamasisha wanawake na
wafanyakazi wa Airtel kuzifikia ndoto zao. Kama tunavyofahamu wanawake wanayo
majukumu makubwa ya familia na kazi, hivyo kuwa na changamoto kubwa ya
kugawa muda wao kwa ufanisi. kwa kupitia Airtel Divas tunashirikiana kwa pamoja
kupeana ujuzi na mawazo ya namna ya kupambana na changamoto hizi na kufikia mafanikio
katika malengo tuliyojiwekea.
Sambamba na hilo tunawahamasisha wanawake
kushiriki katika kujitolea na kutoa msaada kwa jamii na ndo maana leo
tumewaalika kina mama hawa wenye ulemavu na kuwapa nafasi ya kuuza bidhaa zao
na kiasi cha pesa watakachopata leo tutakiongeza mara mbili na kuwawezesha
kupata fedha za kutosha kulipia banda katika maonyesho ya sabasaba. Tunaamini
kwa kufanya hivi tutawawezesha kukuza biashara yao. Natoa wito kwa watanzania
watakaopata nafasi ya kwenda kwenye maonyesho haya wapate nafasi ya
kuwatembelea na kuwaaunga mkono pia.
Akiongea mara baada ya kukabithia msaada
huo mwenyekiti Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania
SWAUTA bi Stella Jairosi Alisema, Tunawashukuru Airtel kwa kutuwezesha kupata
banda zuri liliopo eneo zuri katika maonyesho ya Sabsaba, kwa miaka 8 sasa
tumekuwa tukishiriki katika maonyesho haya lakini hatukuwahi kuwa na banda letu
wenyewe. Kupitia msaada huu kutoka Airtel kutatupatia mwanya wa kuonyesha
bidhaa zetu na kupata mwaya wa kuuza kwa soko la ndani na la nje na pia
kutatusaidia kuuza bidhaa zetu kwa kiasi kikubwa na kuongeza pato letu na hivyo
kuendeleza miradi ambayo hatukuweza kuifanya kutokana na uhaba wa fedha.
Kwa upande wake mgeni rasmi na Mkurugenzi
Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro alisema“ nimejisikia
furaha kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya leo na napenda kuwapongeza sana
Airtel Divas kwa kujitolea kusaidia jamii kupitia shughuli hizi za huduma kwa
jamii wakiwemo wa mama hawa wa kikundi cha walemavu nawahamasisha muendelee na
juhudi hizi.Pamoja na hayo pia nachukua nafais hii kuwahimisha Airtel Divas
kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha uwezo wao katika maeneo yao ya kazi ili
waweze kupata nafasi nyeti katika Uongozi
No comments:
Post a Comment