Tangazo

September 18, 2014

Airtel yazindua Mnara wa Mawasiliano Mbulu mkoani Manyara

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mnara wa  huduma za Mawasiliano  katika kijiji cha Aicho wilayani Mbulu Mkoani Manyara ambapo sasa wakazi wa kijiji hicho na jijini vya jirani wameunganishwa na huduma za simu za mkononi za Airtel. Akishuhudia ni Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala  pamoja na wakazi wa Kijiji  hicho.
 Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brightone Majwala  akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri wakati wa uzinduzi wa Mnara wa  huduma za Mawasiliano  katika kijiji cha Aicho wilayani Mbulu Mkoani Manyara. Pichani ni wakazi wa Kijiji  hicho

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imewawezesha wakazi wa kijiji cha Aicho  na vijiji vya jirani kupata huduma za mawasiliano kufatia uzinduzi wa mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Aicho kata ya Marang wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara

Uzinduzi huo ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuboresha upatikanaji wa mawasiliano na kuwawezesha wakazi wa maeneo ya pembezoni mwa nchi kupata huduma ya mawasiliano ya simu za Mkononi

Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika mkoani Manyara Meneja Mauzo kanda ya kaskazini wa Airtel Bwana Brighton Majwala alisema “ Airtel Tunatambua kuwa mawasiliano ni kichocheo kikuu cha uchumi katika nchini na jamiii yoyote ile, ndio maaana tumeona ni vyema kufikisha mawasiliano katika maeneo yenye changamoto za mawasiliano hususani ya vijijini. Na leo tunazindua huduma za mawasiliano katika kijiji  cha Aiko na kuwawezesha wakazi wa hapa na maeneo ya jirani kupata huduma mbalimbali ikiwemo za kifedha za kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo kwa njia rahisi, salama wakiwa  mahali popote  kwa kupitia huduma ya Airtel Money”.

“Airtel tumejipanga na tutaendelea kutekeleza  dhamira yetu ya kutoa huduma bora za kibunifu na za bei nafuu na huku tukiendelea kuboresha upatikanaji wa mawasiliano katika maeno mbalimbali ya pembezoni nchini”  aliongeza Majwala

Kwa upande wake mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbulu Joseph Geheri alisema” Tunashukuru sana Airtel kwa kuendelea kuboresha mawasiliano na kuwapa vijana wetu kufaidika na kupata Ajira kwa kupitia huduma hizi zilizosheheni hapa wilayani Mbulu.Kadhalika mawasiliano haya yamewawezesha wanafunzi kupata taarifa za matokeo yao ya mtihani ya kuhitimu kwa kupitia simu za mkononi mahali popote pale walipo.

Vilevile tunafurahi kuona jinsi gani Airtel imerahisha mawasiliano haya kijiji hapa na kuwezesha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wakati na kirahisi zaidi, kwa wafanyabiashara,  wakulima pamoja na wafugaji mawasiliano haya yatawawezesha kuendesha shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi zaidi na kupata masoko katika sehemu mbalimbali za nchi kupitia mtandao huu wa simu za mkononi wa Airtel.  Nachukua nafasi hii kuwaasa wakazi wa hapa kuyatumia mawasiliano haya kwa faida yamaendeleo yao na ya jamii kwa ujumla Aliongeza Geheri Airtel inaendelea kupanua wigo  wa mawasilano nchini ambapo wiki zilizopita Airtel ilizindua mnara wa mawasiliano katika mkoa wa Sigunga Kigoma na Muhukuru  Songea , huku ikiwa na  mpango mkakati wa kuzindua huduma za mawasiliano katika maeneo mengi zaidi nchini. Sasa wakazi wa sigunga, Mahukuru na Aicho wanafurahia huduma mbalimbali za Airtel ikiwemo ya kifedha ya Airtel Money Hatoki Mtu hapa, Switch on huduma ya internet  na  vifurushi vya Airtel yatosha na vingine vingi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Airtel launched telecommunication services in Mbulu Manyara Airtel Tanzania has launched a telecommunication service in Aicho Village in Mbulu district Manyara to enabled resident of Aicho and its neighboring village to have access to mobile communication services.

Communication service launch is a continuation of Airtel’s Commitment to widen it network coverage while enhance its communication services in remote areas in order to reach people who lives in the rural part of the country.

Speaking during the launch event,  Airtel Zonal Business Manager Brighton Majwala said” Airtel acknowledge the role of communication in economy development and that Communication is the catalyst of  economy growth  of any nation and community hence we have seen it is vital  to
extend our network coverage to areas face communication challenges, our focus been in rural.

Today we are happy to launch our communication services here at Aicho village, now the resident of Aicho and neighboring hood will have access to our vast products and services including financial services that will enable them to send and receive money across the country, pay utility bills in a secured, reliable and convenient manner through our Airtel Money Service.

We will continue with our commitment to offer quality, innovative and affordable service while expand our network coverage across the country.  What has been demonstrated today is just a continuation of our efforts to offer reliable telecommunication services in Tanzanian Market.

On his side the guest of honor Mbule District Acting Executive Director Joseph Geheri said” we would like to thank Airtel for their continuous efforts in enhancing communication services at Mbulu District. Having number of Airtel sites at Mbulu District has created lots of opportunity including employment to our youth.

Moreover access to information has been made easier, now our student can retrieve their final National Exams results through their mobile phones anywhere any time. Business man, farmers and pastoralist will effectively run their day to day activities, receive information and find market for their products via mobile phone services.  This is a great milestone and I would like to appeal to our people to effectively use the communication service launched today. Added Geheri

Airtel launched its communication service at Sigunga Kigoma and Muhukuru Songea last month, ustomers from those areas and Aicho Manyara will now enjoy ongoing Airtel Offer including Airtel Money Hatoki Mtu Hapa, Switch on Data service, Yatosha Bundles and so many more.

No comments: