Tangazo

September 15, 2014

Airtel yazindua Xpress Shop Dodoma Mjini

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema (kati) akikata utepe kuashiria kulizindua rasmi duka la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu mkoani humo. Anaeshuhudia wakwanza kulia ni mkurugenzi wa airtel huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba na Meneja biashara wa Airtel Dodoma Bw, Stephen Akyoo wakwanza kushoto, Airtel imefanya uzinduzi wa duka hilo jana baada ya kuzindua maduka mengine  katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya  Morogoro,Bukoba na Zanzibar pia yanatarajiwa kuzindulia mwezi huu.
Meneja Mauzo wa Airtel Mkoa wa Dodoma Bw Stephen Akyoo akiwa na wafanyakazi wengine wa Airtel Dodoma akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi. 
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi (katikati), akiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa Mteja Airtel, Bi Adriana Lyamba  (kushoto) na Meneja wa Duka hilo mkoani hapo Bi Elida kulia wakikata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel mtaa wa Mkuu mjini Dodoma jana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akiongea na wananchi na wanahabari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Dodoma barabara ya mkuu Jana.
Wafanyakazi wa Airtel mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Airtel kufungua Duka jipya mkoani hapo mtaa wa Mkuu jana, picha na mpigapicha wetu.
XXXXxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


* Wateja wa Airtel kupata huduma bora na za uhakika Dodoma, Tanzania Septemba 12, 2014.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imefungua duka lake la Dodoma kufatia ukarabati uliokuwa unafanyika wa kuliweka duka hilo kuwa la kisasa zaidi ili kuweza kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora zaidi.

Uzinduzi wa duka hilo ulifanywa na  mkuu wa mkoa wa dodo dkt Rehema Nchimbi ambapo amewapongeza Airtel kwa mpango kabambe wa  kuboresha maduka yake nchini  pamoja na duka la Dodoma.

 Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba alisema,"Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma mbalimbali.

Kwa kupitia duka hili wateja wetu watafurahia huduma zetu za pesa mkononi za Airtel Money ,internet na kuweza  kununua muda wa maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na huduma nyingine nyingi.

Sasa wateja wetu wanauhakika wa kupata huduma bora  kwa haraka zaidi kupitia duka hili. Tutaendelea kutoa huduma za kibunifu zenye uhakika na zenye ubora wakati wote kupitia mtandao wetu bora na mpana ulioenea zaidi nchini.

Lengo letu ni kuhakikisha tuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu na kufikia matarajio yao. aliongeza Lyamba Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Dkt Rehema Nchimbi alisema" nawapongeza sana Airtel kwa juhudi hizi za kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini.

Sote tunatambua mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi nachukua fulsa hii kuwaomba wakazi wa Dodoma watumie vyema nafasi hii kupata huduma bora zitakazorahisisha uendeshaji wa Shughuli zao mbalimalbali za kila siku".


"Serikali inaunga mkono juhudi  zinazofanywa na Airtel na kuwaomba waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasilaino nchini.  Tuko tayari kushirikiana Airtel katika kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za  mawasiliano na hatimaye kuwa maisha bora."

Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni imezindua maduka Morogoro, Bukoba na Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Septemba.

No comments: