Tangazo

September 14, 2014

NSSF YADHAMINI PAMBANO LA SIMBA NA NDANDA FC

NSSF  kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme yadhamini mechi ya kujipima nguvu kati ya Simba ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara  kwenye uwanja wa CCM  wa Nangwanda Sijaona na kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki wa soka mkoani Mtwara.


Mchezo huo pia ulikuwa ni sehemu ya sherehe  za Ndanda Day ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali uliisha kwa matokeo ya timu hizo kutoka suluhu.

NSSF kupitia mpango maalum wa wakulima schemes wenye lengo la kuandikisha na kuhudumia wakulima kwenye mfuko ya hifadhi ya jamii nchini ili kuwawezesha wakulima wote nchini wawe kwenye mfuko wa huo  kupata pensheni ya uzeeni pindi watakapo fikisha umri wa miaka 55 na kuendelea wakulima  hao wataweza kulipwa penshion zao hadi watakapo fariki.

Mpangu huu unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa NSSF wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea.

Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza kulipia kwa mwaka mzima, miezi anayoweza lipia, lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.

NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya  bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za matibabu kwenye familia.

NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto wanne mwanachama na  mwenza.matibabu haya wanapata pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu wa SHIB wa  NSSF na kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu.

NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama 63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani mtwara ambazo ni Tandahimba,Nanyumbu,Masasi ,Nachingwea,Newala,Mtwara Vijijini ambao wengi ni wakulima wa  zao korosho.

Pia kwa akina mama wanapata mafao ya uzazi,kabla na baada ya kujifungua.aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu,pembejeo,dhana mbali mbali za kilimo ili kujiinia kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans.

Ofisi ya NSSF Mkoa wa Mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion  1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasiriamali, wakulima na wafanyakazi.
 Wachezaji  wa  Simba na Ndanda FC wakiingia Uwanjani wakati wa mchezo wa maalum wa kusherehekea Ndanda Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara  na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme. Timu hizo zilitoka suluhu. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akisalimia na timu ya Ndanda FC kabla ya mchezo wao na timu ya Simba uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Mashabiki wa soka wakifuatilia pambano la Simba na Ndanda FC.

No comments: