Tangazo

September 28, 2014

TBL YATOA MSAADA WA VISIMA VYA MAJI MBAGALA NA ZANZIBAR


Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Zanzibar Samir Manji ( wa tatu kushoto),  akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 51 wananchi wa majimbo ya Chumbuni na Mpendae ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa ajili ya mradi wa uchimbaji wa visima vya maji safi na salama katika majimbo hayo juzi. Wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu.
Mwakilishi wa Mauzo ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Bw. Alen Mwebuga (kushoto), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table Maternity Home, Dkt. Baturi Luhanda, mfano wa Hundi ya sh. Milioni 20, kwa ajili ya kusaidia kuchimba kisima cha maji. Wengine katika picha ni Afisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), Mhandisi wa mradi huo, Bw. Onesmo Zakaria na Rais wa Rotary Klab Agnes Batenga. (Na Mpigapicha Wetu)

No comments: