Tangazo

September 24, 2014

UN WAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KUJADILI USHIRIKIANO‏ BAINA YAO

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuboresha ushirikiano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini UN lakutana na wanahabari kujadiliana na kudumisha ushirikiano wao katika habari ambapo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamekuna na viongozi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ili kujadili kwa pamoja.

UN wameeleza kazi zinazofanywa na shirika hilo ili waweze kushirikiana kwenye mambo mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, elimu na kuzifahamu kazi za mashirika hayo hapa nchini.

Hivyo waandishi na wahariri wa habari wameombwa kudumisha ushirikiano katika kazi zote zinazofanywa na mashirika yanayosaidia nchini kwa kiasi kikubwa.

Pia wameweza kuzungumzia ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka kwa kasi sana hivyo kuwataka kuweza kuandika habari zinazowajuza jamii ili kuweza kuuepuka.

Nia na madhumuni ya mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari ni kuweza kujenga ushirikiano madhubuti baina yao na kuweza kushirikiana kwa karibu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wahiriri wa vyombo vya habari nchini ambapo alielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ikiwemo utekelezaji wa agenda mbalimbali za malengo ya milenia.
Bwana Clioni akiendesha mjadala baina ya viongozi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akitoa salamu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa mkutano wa kuendeleza ushirkiano baina ya Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari nchini.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akitoa shukrani kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati walipokutana na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuboresha ushirikiano na mahusiano baina yao.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mkutano huo baina ya Umoja wa Mataifa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kuboresha mahusiano baina yao na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.Untitled
Mkutano ukiendelea huku wengine wakipitia makabrasha mbalimbali yenye taarifa za Umoja wa Mataifa.
Mmoja wa wahariri, Masyaga Matinyi akihoji swali kwa viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano huo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuboresha mahusiano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mashirika ya umoja wa mataifa nchini.

No comments: