Tangazo

September 28, 2014

ZIARA YA KINANA KATIKA JIMBO LA MLALO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Kwekangaga ikiwa siku ya pili ya ziara yake katika wilaya Lushoto ambapo alishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo la ofisi ya tawi la  Kwekangaga ambayo imesema ujenzi wa ofisi hiyo ungegharimu shilingi milioni 45 za kitanzania ,Katibu Mkuu aliigomea taaraifa hiyo baada ya kupata ukweli kuwa ofisi hiyo ingegharimu shilingi milioni nne na nusu tu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM  tawi la Kwekangaga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akisikiliza kwa makini baadhi ya maswali kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Mlalo,Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangamana mwisho kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo la Mlalo uliofanyika kwenye kata ya Lukozi wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Lukozi wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Mtumbi ambapo aliwaambia ni muhimu sana wananchi kushiriki katika maendeleo yao kwani hakuna mtu kutoka nje anaweza kuwaletea maendeleo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusomba kifusi  wakati wa ujenzi wa maabara wa shule ya sekondari Mtumbi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia Wazee wa kijiji cha Sunga
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia wananchi mkono wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara kijiji cha Sunga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama (katikati) na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa eneo la mkutano Sunga.
 Wananchi wa Sunga wakifuatilia mkutano wa Kinana
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Sunga .
 Nape Nnauye akiwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara kata ya Sunga
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Sunga.
Kinana ni Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kufika kata ya Sunga,jimbo la Mlalo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Sunga ambapo alisisitiza kuwa matatizo mengi yanayowakabili wananchi hayo yapo kwenye uwezo wao na wilaya kwani majibu yapo hapo hapo na kuwaambia wananchi hao kuchagua viongozi waadilifu.
 Mwananchi wakifuatilia kwa umakini mkutano wa hadhara wa CCM Jimbo la Mlalo ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia umati wa watu.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Ndugu Twaha Amir Hamza aliyekuwa akiuliza maswali juu ya matatizo ya mipaka kati ya kijiji cha Sunga na Kwentungi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Sunga.
Katibu Mkuu wa CCM ameanzisha utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kwenye mikutano yake ya hadhara ambapo amekuwa akipata maswali, ushauri au maoni ambayo pia hupatiwa majibu na Viongozi husika.
 Umati wa wakazi wa Sunga uliofurika kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wasanii wa kata ya Sunga wakifanya igizo lao baada ya Viongozi kumaliza hotuba, wasanii hao wasanaa ya vichekesho wanafahamika kwa jina la K Square Komedi.

No comments: