Tangazo

September 25, 2014

Ziara ya Kinana Korogwe

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kulima shamba la mpunga kwenye mradi wa kilimo kwanza wa Skimu ya Mahenge.
 Mifereji ya maji kwenye shamba la skimu ya Mahenge
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kufyeka majani kwenye eneo la soko la sabasaba mjini Korogwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kujenga zahanati Mahenge kwa Mndolwa.
Mbunge wa Korogwe mjini Bw. Yusuph Nassir akielezea mipango ya maendeleo ya jimbo lake wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya Mahenge Kwamndolwa .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa vyumba vya maabara vya shule ya sekondari ya Old Korogwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mazoezi ambapo aliwaasa vijana kuwa makini na wanasiasa wanaotanguliza madaraka kuliko utu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa Korogwe walifurika kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua viongozi bora kwenye chaguzi zote zijazo,kuhakikisha watoto wao wanaenda shule na wasirudishwe kwa sababu ya ada na mwisho aliwasisitiza wakazi wa Korogwe kujiunga na mifuko ya Afya ya jamii.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo kusalimia wananchi wa Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mazoezi.
 Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mheshimiwa Mrisho Gambo akiwahutubia wakazi wa Korogwe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi ya Mazoezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Korogwe kwenye mkutano uliokuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa na shauku ya kuuliza maswali kuhusu maendeleo yao ya Korogwe.(Picha na Adam Mzee)

No comments: