Tangazo

October 6, 2014

Airtel Tanzania yazindua na kushereheke Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Bw Sunil Colaso akiongea na wafanyakazi wote pamoja na wanahabari leo hii (hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo katika makao makuu ya Airtel, Airtel inaadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
Wakurugenzi wote wa Airtel wakiongozwa na mkuu wao Sunil Colaso kati wakikata leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaadhimishwa duniani kote kuanzia tareh 6, Airtel imejipanga kuadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso (kushoto)akifuatiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba na Mkurugenzi Mkuu wa Bisahara wa Airtel Bw Mustafa Kapasi wakikata leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaadhimishwa duniani kote kuanzia tareh 6, Airtel imejipanga kuadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba akiongea na wafanyakazi wote pamoja na wanahabari (hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo katika makao makuu ya Airtel, Airtel inaadhimisha wiki hii kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Dar es salaam

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel imejipanga kikamilifu kushehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kuzitambua jitihada na michango ya watoa huduma wao na kutambua
umuhimu wa wateja.

Airtel leo imefanya uzinduzi wa wiki hiyo na kuungana na ulimwengu mzima kusherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja. Airtel inaisherehekewa wiki hii kipekee kabisa kwa kuhakikisha inatembelea
wateja wao na kuendelea kuwapatia huduma bora zenye viwango vya hali ya juu huku wakiongozwa na kauli mbiu ya "Mimi ni Airtel niko hapa kukuhudumia" A am Airtel here for you".


Kitengo cha Airtel huduma kwa wateja kimedhamiria kuitumia wiki hii kujifunza changamoto tofauti toka kwa wateja pamoja na kuwapatia wateja wao wa nje na ndani huduma stahiki kwa staili ya kipekee kabisa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja katika makao makuu ya Airtel nchini Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “kwetu sisi Airtel wiki ya huduma kwa wateja
tunaithamini na kuisherehekea na wateja wetu tukiwekea mkazo katika mambo muhimu tunayotakiwa kuwafanyia wateja wetu kila wakati na sio tu ndani ya wiki hii”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba alisema tunaanza kuisherehekea wiki hii hadi tarehe 10 octoba mwezi huu, wiki itaambatana na mambo mengi yatakayofanywa na wafanyakazi wote wa Airtel kwa lengo la kumfaidisha mteja

Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali na mameneja wao wako katika baadhi ya maduka yetu pamoja na sehemu muhimu za kuhudumia wateja kwaajili ya kukutana na wateja na kuwahudumua  kwa wiki nzima alisema Bi, Lyamba

Katika duka letu kuu Moroco Dar es salaam wateja wiki hii watahudumiwa na mimi mwenyewe na timu yangu ya huduma kwa wateja alisisitiza Bi Lyamba

“Lengo ni kumuhudumia mteja kwa ukaribu zaidi pamoja na kuwashukuru sana kwa kuwa wateja wetu kwa muda mrefu na wakati mwingine kuwa wavumilivu kwetu”,

Kwa kuongezea kipindi hiki cha wiki ya huduma kwa wateja, Airtel inatoa bidhaa bora kwa OFA zikiwemo simu zetu za Tecno H5 android smartphone. Simu hizi zimeshushwa bei na zinatoka zikiwa na OFA kabambe ya kifurushi cha intaneti maalum.



Airtel Tanzania ndani ya wiki hii ya huduma kwa wateja pia imetangaza kuwepo kwa motisha kwa watoa huduma wote wa Airtel kwa lengo la kuwahamasisha kuendelea kutoa huduma bora.

No comments: