Tangazo

October 6, 2014

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


Simu ya Upepo   : “N G O M E”                   Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463             Sanduku la Posta 9203,
Telex                       : 41051                               DAR ESSALAAM, 06 Octoba, 2014
Tele Fax                 : 2153426
Barua pepe            : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                    : www.tpdf.mil.tz
                               
                                                      Taarifa ya Kifo
Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (TWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali  (mstaafu) Hashimu Said Mtezo kilichotokea tarehe 04 Oct 14 kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.

Alizaliwa Machi 18, 1945 Wilaya ya Dodoma   Mjini na alisoma katika shule ya Sekondari ya Tabora kuanzia mwaka 1962 hadi alipohitimu Kidato cha Sita mwaka 1967.  Alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania tarehe 20 Juni, 1968. AlitunukiwaKamisheniJuni 05,1969.

Katika utumishi wake Jeshini, alihudhuria na kufaulu kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi.  Marehemu Brigedia Jenerali Mtezo amewahi kushika madaraka mbalimbali, Mwambata Jeshi nchini Zimbabwe 1987 hadi 1993, Mkurungenzi wa Mafunzo Makao Makuu ya JWTZ 1993 hadi 2002.

  Hadi anafariki alikuwa amestaafu Juni 30, 2002 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 34. Mazishi yatafanyika tarehe 07 Octoba, 2014 Mbezi Lous.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI HASHIMU SAIDI MTEZO (MSTAAFU) AMINA

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari naMahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
KwaMawasiliano zaidi: 0783 - 309963
  

No comments: