Tangazo

October 28, 2014

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii yatembelea Miradi ya NSSF Kigamboni jijini Dar


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (aliyesimama), akifafanua jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya  Maendeleo ya Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mradi wa nyumba za gharama ya chini wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village', iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE/JOHN BADI


Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanua jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya maendeleo ya Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mradi wa nyumba za gharama ya chini wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village', iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Miradi yote ya NSSF, Mhandisi Kareem Mattaka (wa pili kushoto) akifafanua jambo kuhusu ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda (kulia). Wa (pili kulia), ni  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (wa pili kulia), na  (kushoto) ni Meneja wa Mradi huo, Mhandisi John Msemo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakiangalia namna maji yanavyotolewa chini kwa ajili ya kumimina zege ili kuweka nguzo za Daraja la Kigamboni.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mheshimiwa Said Mtanda (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajab wakati akikagua baadhi ya nyumba za mradi wa Nyumba za Mtoni Kijichi.
Mhandisi Msemo akimumyesho Mheshimiwa Said Mtanda moja ya michoro ya Mradi wa Nyumba za Mtoni Kijichi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Said Mtanda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kamati yake kumaliza ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam mapema wiki hii. Miradi waliyoikagua ni pamoja na ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Nyumba za gharama za chini za Mtoni Kijichi na Mradi wa Makazi wa Dege Eco Village. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajab, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka (wa tatu kushoto) na (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau.

No comments: