Tangazo

November 9, 2014

BURIANI ‘AMIGOLAS’; KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KISUTU, DAR

Marehemu Khamis Kayumbu 'Amigolas'
Marehemu Amigolas (katikati) alipokuwa katika Bendi ya Twanga Pepeta, bendi aliyoitumikia kwa miaka mingi.

Mkurugenzi wa African Stars Entertainment Tanzania  (ASET),  Asha Baraka akiwa msibani. ASET inamiliki bendi ya Twanga Pepeta bendi ambayo Marehemu Amigolas aliitumikia kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni kuhamia katika bendi ya Ruvu Stars.
Rogert Hega, 'Katapilla' akiwa msibani.

Victor Mkambi akiwa msibani.

Mama mzazi wa marehemu, Aisha Suleiman, akilia kwa uchungu.

Mtoto wa marehemu, Sophia Khamisi akiwa amezimia msibani.
Waombolezaji wakiwa msibani.
 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

MAZIKO ya mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ aliyefariki usiku wa kuamkia leo yatafanyika kesho saa 9 alasiri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Amigolas amefariki kwa ugonjwa wa moyo akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa. Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Amigo alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote kufanyika.

Marehemu Amigolas amefariki akiwa na umri wa miaka 42, ameacha mke na watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume. Msiba upo nyumbani kwa mama wa marehemu, Mburahati, Mianzini jijini Dar.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. AMEN!


No comments: