Tangazo

November 12, 2014

Mambo 10 ya kushangaza kuhusu Kujamba



Kwanini tunajamba? Kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu, lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda. Kila mtu anajamba, hata Halle Berry nae hujamba.

1. Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa nyingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu,na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.


Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen,asilimia 21 ni hydrogen,asilimia 9 ni carbon dioxide,asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen. Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans, ambayo ndio ina sulfur ndani yake, sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti, hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa. Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

 
2. Kwanini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu,vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili.Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage, kabichi, soda na mayai.


3. Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.


4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde.
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua.


5. Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya. Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara. Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha kikundu (hemorrhoids).

6. Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini, kwao husalimiana kwa kujamba, na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani, Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya,alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".


7. Ushuzi Unawasha Moto
Kama ilivyoandikwa hapo juu, methane na hydrogen inayozalishwa na ushuzi inaweza sababisha moto.

 
8. Mchwa Hujamba Kuliko Wanyama Aina Zote
Ni ngumu kuamini kuwa mchwa ndo anawajibika na matatizo yetu ya "Global Warming".Mchwa huongoza kwa kujamba kwa wanyama,na hiyo huzalisha gesi ya methane.


9. Ukiubana Ushuzi, Utakutoka Usingizini
Hata ujitahidi kuubana vipi, ushuzi utatoka mara utapokua umepumzika, hasa ukiwa umelala.


10. Watu Hujamba Hata Baada ya Mauti Kuwafika
Maiti huendelea kutoa gesi hadi masaa matatu baada ya mtu kufariki dunia; hii huambatana na milio ya kujamba. Hali hii husababishwa na misuli kusinyaa.

Hii ni kwa hisani ya ODDEE

2 comments:

Anonymous said...

hahahaaa badi nimecheka sanaaa..
Its jack (tulawaka)

John Hans Badi said...

Ni kweli Jack imekaa kama kichekesho lakini ndio ukweli wenyewe kwa mujibu wa watafiti wa mambo... Karibu