Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji,
Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji
uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland
Marekani Jumamosi asubuhi. Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu
ulifanyika salama. Picha na Fred Maro xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba
8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns
Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi
wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu,
umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete
inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa
madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa
kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014
No comments:
Post a Comment