Tangazo

April 24, 2015

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA UNI WI-FI

Afisa masoko wa Airtel bw, Prospa Mwanda akitoa maelekezo ya jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi inavyofanyaka kazi kwa kasi kwa Raisi wa wanafunzi chuo kikuu cha SAUT mwanza Bw, Sogone Wambura (wakwanza kulia) na Makamu wa Raisi wa chuo hicho Bi, Pearl Mecar (kati) mara baada ya Airtel kuzindua huduma hiyo chuoni hapo jana.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanafunzi wa SAUT Mwanza (hawapo pichani) muonekano wa vocha za huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti iliyozinduliwa chuoni hapo jana maalumu kwaajili ya kuwapa wanafunzi intaneti nafuu na yenye kasi zaidi.
Mshauri wa wanafunzi chuo cha St. Augustine Mwanza (SAUT) akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) kuitumia vyema huduma iliyozinduliwa na Airtel ya Wi-Fi intaneti ili kutimiza uhitaji wao katika masomo na kuongeza ufaulu chuoni hapo. Hafla ya uzinduzi ilifanyika chuoni hapo jana.
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga (kulia), akiwa ameshikilia bango linaloonyesha huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti  maalum kwa wanavyuo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza Mwanza katika chuo cha St Augustine (SAUT) pamoja nae anaefuata ni raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura, Mshauri wa wanafunzi chuoni hapo bw,Liberates Ndegeulaya na Afisa masoko wa Airtel Mwanza Bw, Emanuel Raphael.
    
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

· Wanafunzi chuo kufurahia Uni Wi-Fi kwa kifaa kinachotumia Wi-Fi
· Uni Wi-Fi ya Airtel kupatikana kwa laini ya mtandao wowote

MWANZA
Kampuni ya simu za mkono ya Airtel Tanzania katika muendelezo wa kutoa huduma bora na nafuu nchini imezindua huduma mpya ya kisasa ya UNI Wi-Fi itakayowaweza wanafunzi vyuoni kufurahia huduma ya Intaneti yenye kasi zaidi
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika chuo kikuu cha SAUT Mwanza Meneja Mauzo wa Kanda ya Ziwa Bw, Raphael Daudi alisema “huduma ya Airtel UNI Wi-Fi tumeianzisha kwaajili ya kuwapatia wanafunzi huduma nafuu ya intaneti yenye kasi zaidi wakati wanapofanya shughuli zao za masomo au wanapoingia katika mitandao ya jamii kupata taarifa mbalimbali muhimu”
Ulimwenguni Intaneti sio kitu cha anasa tena na pia kutokana na  kasi ya  uhitaji wake kwenye mambo ya maendeleo ya uchumi na kijamii kwenye makundi tofauti vikiwemo  vyuo vya elimu ya juu Airtel tumeona ni vyema  kuja na ubunifu huu kuleta suluhisho kwenye kuwahudumia wateja wetu”
Leo huduma ya intaneti kupitia Airtel UNI Wi-Fi hapa Chuo cha St, Augustine Mwanza (SAUT) ni rahisi na nafuu kabisa kupitia Airtel
Kwa Upande wake Meneja Masoko wa Huduma hiyo Bi, Aneth Muga amesema “Airtel Uni Wi-Fi tunayozindua leo nimuendelezo wa mikakati yetu ya Airtel kutoa huduma nafuu kwa wanafunzi,  mwishoni mwa mwaka jana pia tulizindua Uni 255 vocha kwenye vyuo mbalimbali ili kuwapatia huduma ya bando za Intaneti, SMS pamoja na muda wa maongezi nafuu zaidi kuliko zote”
Leo hii Wi-Fi vocha ipo ya Siku, Wiki, Mwezi au bando la usiku kwa gharama nafuu ya hadi shilingi mia tano kwa GB 1 kwa siku.
Unachotakiwa kuwa nacho ili kufaidi huduma hii ni kuwa na kifaa chochote kinachoweza kutumia Wi-Fi kama vile smartphone, laptop, tablet, Camera, printer na utaunganishwa bila kujali unatumia laini ya Airtel au mtandao wowote.
“Leo tumeanzia hapa SAUT lakini tutahakikisha inasambaa vyuoni kote na baadae nchi nzima ili vijana na wale wote wanaokwenda na wakati waweze kufaidika nayo katika matumizi ya kimtandao” alimaliza kusema Bi Muga
Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa Chuo hicho Bw, Liberatus Ndegeulaya alisema “hapa chuoni SAUT tumefarijika sana kuona Airtel mara zote mnaanzia kwetu mnapotaka kuzindua huduma hizi rafiki kwa mawasiliano. Kwa elimu ya sasa hii Wi-FI ni muhimu sana inarahishia wanafunzi wetu na hata sisi walimu katika ufundishaji”
Natoa wito kwa wanafunzi wote kuitumia Airtel Wi- Fi kama nyenzo ya kufikia mmalengo ya elimu yao
Nae Raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura aliishukuru Airtel huku akiitikia wito wa kuitumia huduma hiyo kwa manufaa ya kupandisha kiwango cha elimu nchini  sambasamba na ukuaji wa teknolojia mbalimbali.
“Asanteni Airtel kwa ubunifu huu na kuleta Airte Wi-Fi sisi wanafunzi tutahakikisha tunajiwekea utaratibu wa kuitumia katika utaratibu unaofaa na wenye manufaa ya kwa elimu nan chi yetu’ alisema Wambura Raisi wa wanafunzi SAUT

No comments: