Tangazo

April 28, 2015

Wanafunzi 60,000 wa UDOM kufurahia Airtel WI-FI

Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti  inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu.
Meneja masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya Airtel kuzindua huduma yao ya  intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi  maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho jana.


Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

• Pia Airtel yazinduzi mnara wa pili UDOM

Dodoma, 

Kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu 

UNI WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na  kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya wanafunzi na  pia tumeongeza mnara wa pili  wa simu   ambao tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi  wa nchi yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya "

Tunafuraha kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni  kwani spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari mbalimbali za  taaluma au kijamii  kupitia mtandao wetu wa Airtel "

Meneja Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa  UDOM, kwa kutumia simu zao za mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia. 

Wanaweza kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana  masaa 24 , kwa kifurushi cha siku , wiki,  mwezi na kifurushi cha usiku mzima.

Fikiria! Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi  500 tu! Alisisitiza Bi, Muga.

Kwa upande wake mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM) Bw, Dick Manongi   alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni. Nina hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea wanafunzi  urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa nchini na hata nje ya nchi ".

Ningependa kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza ujuzi wao kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae.

Uzinduzi wa Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya Airtel Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint Augustine (SAUT) jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia vyoo vingine hapa nchini.

No comments: