Tangazo

June 22, 2015

Airtel FURSA yawawezesha Vijana Wajasiriamali Dar

Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (wa pili kulia ), akimkabidhi zawadi ya mashine ya kushonea 'cherehani', kwa Betha Benedict (wa pili kushoto), mkazi wa Bunju Jijini Dar es Salaam baada ya kuwezeshwa na mpango wa Airtel Fursa “Tunakwezesha”. Kushoto ni mama yake Betha na kulia ni Meneja wa Airtel, Fadhili Mwasijeba.
Bertha Benedict (watatu Kulia) akionyeshwa na meneja Huduma wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wapili Kulia) vifaa alivyokabidhi na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kushoto ni   Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wa Airtel Fursa,  mama yake Betha na kulia ni Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kusini, Fadhili Mwasijeba.


Wafanyakazi  wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Bertha Benedict (wapili Kulia) mara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kutoka kushoto ni Irene Paul balozi wa Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, mama yake Bertha, Hawa Bayumi na Meneja mauzo wa Airtel  kanda ya kusini , Fadhili Mwasijeba.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

DAR ES SALAAM 

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambao umelenga kuwawezesha vijana wajasiliamali wadogo wadogo nchini umetoa msaada mwingine tena jijini Dar es salaam kwa msichana mjasiriamali Bertha Benedicto.

Bertha ambaye amelelewa katika Kituo cha Kulea watoto cha Dogodogo Center Kilichopo Bunju Jijini Dar es Salaam na kuhitimu mafunzo ya mwaka mmoja ya ufundi wa kushona nguo kituoni hapo amepatiwa vifaa mbalimbali pamoja na cherehani ya kisasa ili kuendeleza ujuzi wake.

Akiongea wakati wa makabithiano Meneja wa mahusiano ya jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema  “ Airtel tumeona ni vyema kupitia mpango wetu wa Airtel Fursa kumpatia vifaa na mashine hii ya kisasa ya kushonea Bi Bertha Benedecto  kwa lengo la kumwezesha kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa ufanisi zaidi.  

Sambamba na hilo  tumeweza kumpeleka kwenye mafunzo ya kumsaidia  kujijenga, kuweka mahesabu yake na kuendesha biashara yake ili aweze kukuza biashara na kuisaidia familia yake”. 

Tunaamini hii ni nafasi ya pekee kwa vijana wadogo kati ya umri wa miaka 17 mpaka 24 walioko katika maeneo mbalimbali ya nchi kuweza kufaidika na mpango huu wa Airtel Fursa wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali wadogo wadogo kukuza mitaji na biashara zao kwa ujumla". Aliongeza Bayumi

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Bertha amesema vifaa hivyo vitamwezesha kuendesha maisha yake na familia kwa ujumla huku Mama yake Immaculate Makinda akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.

Bertha alisema, “nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu. Kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa. Nimekuwa nikipata ugumu wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu lakini sasa naamini nitapata wateja wengi sana na kuinua biashara yangu”

Kwa upande wake Mratibu wa Dogodogo Centre, bw.Issa Buzohela alisema, anaiomba kampuni ya Simu ya Airtel  kuendelea kukisaidia kituo hicho na kuinua vipaji vya vijana kwani nchi yetu imezungukwa na vijana wenye vipaji mbalimbali lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipaji vyao.

Mpaka sasa Airtel Fursa  imeshawawezesha vijana mbalimbali na kuboresha shughuli zao za kiuchumi kwa kuwapatia vitendea kazi  na kuwaingiza katika warsha za mfunzo ya Airtel Fursa ili waweze kutimiza ndoto zao.

No comments: