Tangazo

June 4, 2015

NEMBO Govt

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
nembo%20ya%20NEC

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

MIKOA YA
GEITA, SIMIYU, MWANZA, SHINYANGA, ARUSHA , KILIMANJARO, MARA NA MANYARA .

Zoezi hilo la Uboreshaji litanzia tarehe
09/06/2015 hadi  09/07/2015.
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji katika Kata zote za Mikoa hiyo mine iliyotajwa.
Vituo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
·      Waliotimiza umri wa Miaka 18 na watakaotimiza Miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba 2015.
·      Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
·      Wote ambao wanazo sifa lakini hawajawahi kujiandikisha
·      Wananchi wanatakiwa kwenda kujiandikisha kwenye vituo vya kujiandikisha vilivyoko ndani ya Kata zao.
Uandikishaji utafanyika kwa muda wa siku saba (7) kwa kila kituo.
JITOKEZE SASA NENDA KAJIANDIKISHE
Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, +255 772 55 55 53

S.L.P. 10923, Dar es Salaam

No comments: