Tangazo

June 21, 2015

ZIARA YA KINANA YAWA NA MAFANIKIO MKOANI GEITA

 Wakazi wa Kalangalala wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano wake wa mwisho mkoani Geita.
  • Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,pamoja na msafara wake amesafiri umbali wa kilomita 1680 katika ziara yake ya mkoa Geita.
  • Ametembelea jumla ya wilaya tano (5) na majimbo yote sita (6) ya uchaguzi.
  • Amehutubia jumla ya mikutano 78 ikiwemo mikutano 6 ya ndani na 72 ya hadhara.
  • Amekagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kutembelea jumla ya miradi 53 ikiwemo miradi 5 ya Chama na miradi 48 ya Maendeleo ya wananchi
  • Amepokea jumla ya wanachama wapya wa CCM 6,816 wakiwemo wanachama 640 kutoka vyama upinzani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kalangalala,Nyankumbu Geita
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifafanua baadhi ya masuala yanayowasumbua wananchi wa Geita na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kalangalala, Nyankumbu Geita ambapo aliwata wananchi hao kutokubali kuyumbishwa na vyama vilivyopoteza muelekeo.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Geita Mhe.Vicky Kamata akihutubia wananchi wa Kalangalala,Nyankumbu Geita.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwaonyesha baadhi ya viongozi mkoani Geita jinsi habari za ziara ya Kinana zinavyofuatiliwa kwenye mitandao ya kijamii.
 Baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameshikana mikono na Viongozi wa CCM Geita wakati wa kukabidhi baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa Viti maalum Mhe.Vicky Kamata kwa viongozi wote wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake katika kata zote mkoani Geita.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama waliohama uppinzani na kujiunga CCM ambapo zaidi ya wanachama 600 walijiunga na CCM kutokea vyama vya upinzani mkoani Geita.

No comments: