Tangazo

July 8, 2015

BURIANI MWANAHABARI MARIAMU MKUMBARU

Mwandishi wa Habari, Mariam Mkumbaru amefariki dunia.
 
Mkumbaru alifikwa na umauti katika ajali ya gari inayodaiwa kutokea jana Ruangwa, mkoani Lindi akiwa katika shughuli zake.

Simu yake ilipojaribu kupigwa ili kupata ukweli wa tukio hilo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mama yake ambaye hata hivyo alishindwa kuzungumza kutokana na kulia.

Mkumbaru, amewahi fanyia kazi katika vyombo vya habari vya The Guardian Ltd, New Habari, Uhuru, Mzalendo, BBC, na baadae kuandikia mitandao ya kijamii Blogs.

Hadi anafikwa na umauti, alikuwa ni Mshauri wa Mradi wa Mama Yee unaotekelezwa na UTPC kupitia gazeti la Tuwasiliane.

Kifo hicho ni pigo lingine kwa tasnia ya Habari nchini Tanzania kufuatia mfululizo wa vifo vya waandishi vilivyotokea kwa mwaka huu ambapo vinadaiwa kufikia waandishi 7.  
 
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE... AMEN

No comments: