Tangazo

July 26, 2015

GULIO LA MAGARI ‘AUTOMART’ LAZINDULIWA JIJINI DAR


Mkurugenzi wa Vision Investments, Ally Nchahaga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijijini Dar es Salaam Julai 26.2015, wakati wa uzinduzi wa Gulio la Magari lijulikanalo kama ‘Automart’ litakalofanyika kila Jumapili ya mwisho wa mwezi na kuwakutanisha  wauzaji na wanunuzi wa magari katika viwanja vya maegesho ya magari vya Hoteli ya Sea Cliff Masaki jijini.  Kushoto ni Meneja masoko wa Mtandao wa kuuza magari wa Cheki.co.tz, Mori Bencus na Mkurugenzi wa kampuni ya Auto Sport Repairs, Sikandar Merali. PICHA ZOTE NA JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG

Meneja Masoko wa Mtandao wa kuuza magari wa Cheki.co.tz, Mori Bencus (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijijini Dar es Salaam Julai 26.2015, wakati wa uzinduzi wa Gulio la Magari lijulikanalo kama ‘Automart’ litakalofanyika kila Jumapili ya mwisho wa mwezi na kuwakutanisha  wauzaji na wanunuzi wa magari katika viwanja vya maegesho ya magari vya Hoteli ya Sea Cliff Masaki jijini.  Katikati ni Mkurugenzi wa Vision Investments, Ally Nchahaga na Mkurugenzi wa kampuni ya Auto Sport Repairs, Sikandar Merali.

Mkurugenzi wa Vision Investments, Ally Nchahaga (mwenye tisheti nyeupe), akikagua bidhaa mbali mbali za magari kutoka katika baadhi ya makampuni yaliyoshiriki katika uzinduzi huo.
Baadhi ya magari yaliyoletwa katika gulio hilo kwaajili kuuzwa.


DAR ES SALAAM

Kwa mara ya kwanza Tanzania Vision Investments inawaletea Automart mbadala sahihi wa kutimiza mahitaji yako yote ya magari. Gulio la Kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wauzaji na wanunuzi wa magari watakutana katika mazingira rafiki.

Makutano  haya baina ya wateja kwa wateja na wanunuzi na wateja;yatafanyika katika viwanja vya Sea Cliff Hotel, Dar es Salaam. Automart itafunguliwa tarehe 26 July 2015 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 Jioni.

Makutano  haya yameandaliwa kuwapa fursa wanunuzi na wauzaji wa magari binafsi na makampuni tofauti fursa ya kuwa na sehemu moja kwa mahitaji yote. Pamoja na hayo tunaalika huduma shirikishi zikijumlisha kampuni za bima, taasisi za fedha wanao toa mikopo ya magari, Vilainishi vya magari na Kliniki za magari kutoa huduma.

Kwa mtu yeyote anae hitaji kuuza gari lake atachangia Shilingi elfu 50 tu. Ikiwa ni mchango wakuweka gari lake katika viwanja vya Automart na kufaidika na kuwekwa katika mtandao wa cheki.co.tz (tovuti namba 1 ya magari Tanzania pamoja na mitandao ya jamii (facebook) kwa siku 60 baada ya Gulio.

Automart imedhaminiwa na SMS WORX, CHEKI.CO.TZ, AUTOSPORT REPAIRS.

No comments: