Meneja wa Huduma za Ziada wa Airtel,
Prisca Tembo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ya Airtel ‘Jiongeze na
Mshiko’ itakayomwezesha mteja wa mtandao huo kujishindia mamilioni ya pesa kwa
njia ya sms. Kushoto ni na Afisa Huduma za Ziada, Fabian Felician na Afisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
* Yazindua sms promosheni na kuwazawadia wateja wake nchi nzima
* Promosheni itadumu kwa zaidi ya siku 120
Kampuni
ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni kwa wateja wake yenye
lengo la kuboresha uhusiano pamoja na kuwazawadia wateja wake nchi nzima
kila wiki kwa muda wa siku 120.
Promosheni
hiyo ijulikananyo kama " Jiongeze na Mshiko" ni ya kipekee kwani
inampatia mteja kujiunga na kushiriki bure kwa kujibu maswali na kujishinda
shilingi milioni 1 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia shilingi
milioni 2.
Na
ikiwa mteja atapenda kujishindia zawadi kubwa zaidi ataweza kujiunga na
ngazi ya Premium kwa kuchajiwa shilingi 300 kwa siku na kupata
nafasi ya kujishindia shilingi milion 3 kila wiki na mwisho wa promosheni
kujishindia shilingi milioni 50.
Akiongea
wakati wa Uzinduzi wa promosheni hiyo, Meneja huduma za ziada wa Airtel, Bi
Prisca Tembo, alisema" promosheni hii inathihirisha lengo letu la
kuwawezesha watanzania kufikia ndoto zao na huku tukiendelea kutoa huduma
bora za kibunifu zinazokithi mahitaji yao.
Promosheni
ya "Jiongeze na Mshiko" itawawezesha watanzania wengi kujishindia mamilioni
ya pesa kila wiki na kuwawezesha kupata fedha kwaajili ya kuendesha shughuli
zao za kijamii na kiuchumi pindi watakapoibuka washindi kwa muda wa wote wa
mienzi minne.
Mteja
atatakiwa kujibu maswali na kujikusanyia pointi zitakazomwongezea nafasi ya
ushindi na kuweza kujishindia zawadi ya pesa taslimia kupitia promosheni hii ya
" Jiongeze na Mshiko" natoa wito kwa watanzania kujiunga na
kupata nafasi ya kujishidia pesa taslimu kila wiki.
Akiongea
jinsi ya kujiunga na kushiriki , Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde
alisema "wateja wataweza kujinga na promosheni hii bure kwa kutuma ujumbe
wenye neno "BURE" kwenda namba 15470, na kasha kuanza kupokea
maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na
kujikusanyia pointi.
Mteja
atakapomaliza kujibu maswali ya bure atapata ujumbe utakaomuuliza kama
angependa kujiunga na ngazi ya premier, ili kuwezeshwa kufunguliwa maswali
zaidi na kujikusanyia pointi nyingi kwa zawadi zenye thamani kubwa.
Aliongeza
kwa kusema maswali yatakayoulizwa ni ya kawaida hivyo tunategemea wateja wetu
watafurahia kuyajibu na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milioni 108
ikiwa ni moja ya njia ya kuwazawadia kwa kutumia huduma zetu.
Alitoa
wito kwa Tanzania kuwa waangalifu na kuhakiki taarifa zozote wanazopewa
kuhusu Ushindi kwa kupiga 100, namba yetu ya huduma kwa wateja.
No comments:
Post a Comment