Tangazo

October 21, 2015

HEPI BESDEI YA KUZALIWA MDAU ANDREW CHALE

DSC_2549
Leo Jumtano, 21.Oktoba 2015. Ni siku muhimu sana ya kuzaliwa mdau mwanahabari na blogger Andrew Ramadhan Chale (pichani). Tunamuombea kila la heri, Afya njema na maisha marefu na kazi yenye furaha katika kuhabarisha jamii kupitia blog.

Alizaliwa siku kama ya leo 21 Oktoba, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga, Ilala Jijini Dar es Salaam-Tanzania. Anabainisha kuwa, kufikisha miaka 30, leo hii ni jambo la kujivunia kwani amepitia changamoto nyingi za maisha hivyo anamshukuru kila mmoja aliyegusa maisha yake.

Pia mdau anawakaribisha kuungana nae katika tukio maalum la kujumuika pamoja na watoto wa kituo cha Tumaini la Maisha, wanaoapatiwa matibabu ya matatizo ya ugonjwa wa Kansa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Tukio hilo litafanyika kuanzia mchana wa saa nane na kuendelea hadi saa 11, jioni, kutakuwa na utoaji wa zawadi, kufanya shughuli za kijamii za kujitolea na kubadilishana mawazo na watoto/ wazazi na walezi wa watoto hao. Katika eneo la hostel hizo zilizopo ndani ya Hospitali ya Muhimbili.

Kwa wanaoweza kujumuika nae wasiliana nae kupitia Whatsapp 0767076376 ama mpigie 0719076376
wadau mnaweza kuungana kwenye mitandao ya kijanaa kupitia facebook:https://www.facebook.com/anderew.chale

No comments: