Kutoka Kulia;
Afisa Masoko kanda ya Kati, Hendrick Bruno na Meneja Uhusiano wa Airtel
Jackson Mmbando wakisaidiana kuhesabu hela na mshindi wa promosheni ya
Airtel Mkwanjika mkoani Dodoma bw Rioba Matiku (wapili toka kushoto)
pamoja na mtangazaji wa kipindi cha mkwanjika Bw Godfrey Rugalabamu (gala B)
kulia ikiwa ni zawadi yake aliyojizolea katika boxi la Airtel
Mkwanjika mkoani Dodoma jana, hadi sasa tayari Airtel imeshawanyakua washindi
100 na kuwazawadia pesa taslim.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES
SALAAM
Airtel Mkwanjika tayari imeshawazawadia jumla ya watanzanzia 100
tangu ilipozinduliwa ambapo jana washindi wengine watatu kati ya saba
wa Airtel toka mikoa ya Singida,Dodoma na Tabora, wamevuna fedha
katika boxi la promosheni ya 'Airtel Mkwanjika' wakati Boxi la Mkwanjika
lilipofika mkoani Dodoma kwa lengo la kuwazawadia washindi wake wa kanda ya
Kati.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema hayo
katika droo iliyochezeshwa mjini Dodoma jana kwa wateja wa
kanda ya kati ambapo wateja wanne wameshindwa kufika licha ya kuambiwa
watagharamikiwa kila kitu ikiwemo nauli, chakula na malazi ili waweze kufika
kujizolea fedha lakini wamekuwa hawaamini na kuhofia kuwa inawezekana ni
matapeli.
"leo wateja wa Singida,Dodoma na Tabora, ni zamu yenu
kujizolea mapesa ya Airtel Mkwanjika, pia natoa wito kwenu wateja wa airtel
mnapopigiwa simu za ushindi kwa namba ya Airtel 0683-442244 kutoa
ushirikiano kwakuwa droo hiyo haina tozo ya aina yoyote laisema mmbando”.
Mmbando alisema Airtel imetenga kiasi cha sh.milioni 300 kwaajili
ya wateja wa Airtel na kila mmoja anaweza kushinda na mteja anachotakiwa
kufanya ni kujiunga na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza salio
kwa kutumia vocha na kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ya siku bila makato
yoyote.
Alisema
kila siku wateja wanne wa airtel wanavuta mkwanja katika promosheni hiyo na
huchezeshwa kila baada ya siku saba za wiki na kutoa washindi 28.
Alibainisha bado zaidi ya wateja 200 kushindaniwa kwenye
bado droo tisa zilizobaki ambazo zitawapa fursa wateja wanne wa airtel
kila siku kushinda kila mmoja hadi sh.milioni moja.
Wakizungumza mara baada ya kujiokotea fedha katika droo hiyo,
mshindi wa kwanza mkazi wa Dodoma,James Ryoba matiku, alisema ameweza kujipatia
Shilingi laki tisa na elfu kumi ambazo zitamsaidia kuongeza mtaji katika
biashara zake za nguo.
Kwa upande wake, Mkazi wa Tabora, Devota Fongonyo, alisema awali
alipopigiwa simu ya ushindi hakuamini na kuona kuwa ni matapeli lakini baada ya
siku nne alipigiwa tena na akubali kufika Dodoma huku akiwa na hofu.
Alisema katika droo hiyo amejipatia kiasi cha shilingi laki tisa
na elfu thelasini ambazo zitamsaidia kulipa ada za watoto wake.
Naye
Mkazi wa Kongwa, Elias Makani, alisema amejipatia kiasi cha shilingi laki Saba
na elfu tisini ambazo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo.
No comments:
Post a Comment