Mwandishi wa habari wa TBC TV, Oliver akikabithiwa modemu yake ya Airtel
Wingle mara ya kuibuka mshindi katika raffle iliyoendeshwa wakati wa
uzinduzi.
|
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Vicky Kimaro
akikabithiwa modemu yake ya Airtel Wingle mara ya kuibuka mshindi katika
raffle iliyoendeshwa wakati wa uzinduzi.
|
Mwandishi wa habari wa EATV ,Alex Lazaro akikabithiwa modemu
yake ya Airtel Wingle mara ya kuibuka mshindi katika raffle iliyoendeshwa
wakati wa uzinduzi.
|
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Inakuja na ofa ya 5GB BURE, inauwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 10.
· Airtel yaleta modem ya maajabu inayoweza kuunganisha zaidi ya vifaa 10 kwa wakati mmoja.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua modemu mpya ya maajabu itakayowawezesha wateja wake kufurahia huduma za Intaneti na Wi-Fi kwa kuunganisha vifaa zaidi ya 10 kwa wakati mmoja wakiwa mahali popote nchini
Modemu hiyo ya maajabu ijulikanayo kama “Airtel Wingle” imelenga kutatua mahitaji ya huduma za kimtandao kwa watumiaji wake ambapo mahitaji ya huduma za intaneti yamekua kwa kasi nchini na kuifanya Airtel kuleta modem hiyo ya maajabu ili kuwahakikishia wateja wake uhakika wa huduma za kimtandaoni kwa gharama nafuu zaidi nchi nzima
Akiongea wakati wa halfa ya Uzinduzi iliyofanyika katika duka la Airtel Expo lililopo jijini Dar es Saalam, Meneja Uhusiano wa Airtel , Bwn Jackson Mmbando allisema “Tunayofuraha kuzindua modemu hii ya kipekee ya Airtel wingle ambayo huduma zake zinaenda sambamba na dhamira yetu ya kuwafikishia wateja wetu huduma za intaneti zenye kasi zaidi na pia kuwaongezea wateja hao huduma nyingine bora zaidi za Wi-Fi kwa kuwafaidisha wateja wengi kwa modem hiyo hiyo moja wakiwa mahali popote”
Eliakimu alifafanua kuwa “Bila kujali mtandao unaotumia, modemu ya Airtel Wingle itawawezesha wateja wetu kuunganisha zaidi ya vifaa au watumiaji 10 kwa wakati mmoja na kufaidi huduma ya Wi Fi kwa kasi na urahisi. Modem hii ya maajabu yenye Wi-Fi itaweza kutumika na familia, marafiki kwenye ofisini au popote mara tu inapounganishwa kwenye Laptop au katika sehemu yeyote inayoweza kutumia Modem kama vile kwenye gari, soketi za ndani ya nyumba au Hotelini, Televisheni pamoja vifaa vingine vingi vinavyotumia modem”
Akiongea kuhusu upatikanaji wa modemu hiyo, Afisa wa Airtel kitendo cha huduma za Intaneti, Ndevonaeli Eliakimu alisema, Modem ya Airtel wingle inakuja na ofa kabambe ya kifurushi cha Internet cha 5GB kwa mwezi. Tumejipanga kuendelea kutoa huduma za kabambe zitakazowapatia wateja thamani ya pesa zao. Modemu hii ya Airtel Wingle itapatikana katika maduka yote ya Airtel nchi nzima na pia itapatikana katika Duka letu la Airtel Expo kwa bei nafuu yaani OFA kuanzia sasa”
Airtel imezinduzi modemu ya maajabu ya Airtel Wingle ikiwa ni muda mfupi tangu ilipozindua duka lake la kisasa la Airtel Expo jijini Dar es salaam ili kudhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu unaoendana na karne ya sasa ya mawasiliano huku ikitoa huduma hizo kwa gharama nafuu zaidi.
No comments:
Post a Comment