Tangazo

January 19, 2016

MAZISHI YA MKURUGENZI MKUU WA TAA, SULEIMAN SAID SULEIMAN JIJINI DAR



  Jeneza lenye mwili wa marehemu Injinia Suleiman, likifikishwa makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2016 tayari kwa mazishi.
 Marehemu Injinia Suleiman Said Suleiman

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

MKURUGENZI  Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, Injini Suleiman Said Suleiman  amefariki ghafla mapema leo asubuhi Januari 18, 2016, wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya Hindi eneo la Magogoni.

Hayati Injinia Suleiman, amezikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo maelfu ya wananchi walihudhuria wakiwemo viongozi mbalimbali wa taasisi mbalimbali. 

Kwa mujibu wa taarifa za kifo cha injini Suleiman iliyotolewa baada ya mazishi yake, Marehemu alikutwa na umauti wakati akiogelea na ghafla aliishiwa nguvu na kuomba msaada, hata hivyo pamoja na jiyihada za kumuokoa tayari Injinia Suleima alikwishakufa.

Itakumbukwa ya kwamba, marehemu alikuwa ni mwanamichezo mahiri na kuna wakati Fulani alikuwa kiongozi wa Simba na akapewa jina la “Yeltsin” kutokana na msimamo wake mkali katika kutekeleza majukumu yake.

Wachezaji na wapenda soka walifurika kwenye mazishi yake na huzuni ilitawala kila kona kutokana na jinsi marehemu Injinia Said alivyokuwa karibu na watu. Marehemu ameacha mke na watoto watatu.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI AMIN
 Hosam Suleiman Said Suleiman, (kushoto), mtoto wa mwisho wa marehemu akifarijiwa na vijana wenzake
Balozi wa Uholanzi hapa nchini, Jaap Frederiks akijumuika na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam. Uholanzi ni mdau mkubwa wa viwanja vya ndege hapa nchini
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mzee Hassan Dalali, akimuelezea marehemu wakati kuhusu mchango wake katika klabu hiyo
Mfanyakazi wa TAA, akiwa na huzuni wakati wa mkusanyiko wa waombolezaji nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (TAA), ambaye pia anashughulikia Mahusiano, Bw.Ramadhan Maleta, (katikati), akiwa na huzuni wakati wa mkusanyiko wa waombolezaji nyumbani kwa marehemu 
Mwenyekiti wa Bodi ya TAA, Profesa Msambichaka, akitoa salamu za Mamlaka wakati wa mkusanyiko wa waombolezaji nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam

Bw. Maleta, akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa TAA, Bw. Godfrey Lutego, (kushoto)
Salamu kutoka TAA

Mkurugenzi wa mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere TBIII, Mhandisi Mohammed Milanga, (mwenye balaghashia)akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu
 Aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Injinia Prosper Tesha, akimuelezea marehemu ambaye alichukua nafasi yake baada ya mkataba wake kumalizika
 Huzuni ilitawala kwenye mazishi ya Injinia Suleiman
Baadhi ya wadanyakazi wa TAA, wakiwa makaburini wakati wa mazishi hayo

No comments: