Tangazo

March 23, 2016

BHARTI AIRTEL NA AMERICAN TOWER CORPORATION YATANGAZA MAKUBALIANO YA KUUZA MINARA YA MAWASILIANO TANZANIA

New Delhi, India na  Johannesburg, South Africa 

Kampuni ya Bharti Airtel (Airtel) leo imetangaza kuingia makubaliano ya kimkataba na kampuni ya American Tower Corporation (American Tower)(NYSE: AMT), kwa niaba ya kampuni tanzu  ya Airtel Tanzania itakayopelekea kuuzwa kwa minara yake ya mawasiliano takribani 1350 nchini Tanzania. 

Chini ya mkataba huo, kampuni ya American Tower pia itachukua minara mingine  takribani 100 ambayo iko katika hatua ya kujengwa na kuendelezwa ambapo Airtel sasa italipia gharama za kukodi minara hiyo chini ya mkataba wa awali wa miaka 10.

Akiongea kuhusu makubaliano hayo, Christian de Faria, Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Bharti Airtel Africa alisema “ Tunayofuraha kukuza ushirikiano wetu na kampuni ya American Tower barani Afrika.  

Mapendekezo ya makubaliano haya ni mwendelezo wa filosofia yetu ya kuhakikisha tunaachana na utamaduni wa kumiliki rasilimani na kuhamasisha matumizi ya minara ya mawasiliano kwa pamoja ili kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano ambao zitasaidia huduma za mawasiliano kuwa bora zaidi. 

Airtel bado inaendelea na dhamira yake ya kuwekeza katika uendeshaji wa huduma zake Tanzania na kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake nchi nzima’’  

“ Tunayofuraha kubwa kutangaza kuingia katika biashara nchini Tanzania na kuendeleza ushirikiano wetu na Airtel, moja kati ya kampuni  kubwa  ya huduma za mtandao inayoongoza duniani’’ alisema Hal Hess,  Raisi wa American Tower katika ukanda wa ulaya, mashariki ya kati na Afrika  

“Tanzania ni moja kati ya nchi yenye matarajio ya kukua kwa idadi ya watu na kasi kiuchumi ni kubwa ikiwa ni sawia na nchi nyingine za Afrika tunazoendesha biashara zet,hivyo Tanzania inakua ni kivutio kikubwa cha uwekezaji kwetu.

Mauzo ya minara ya mawasiliano itaiwezesha Airtel kuwa makini na kuongeza ufanisi kwenye kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake,na vile vile kupunguza madeni na gharama za uendeshaji wa minara kwa kiasi kikubwa.

Makubaliano ya mkataba huo yanategemewa kufungwa katika kipindi cha kwanza cha mwaka 2016.

No comments: