Tangazo

March 15, 2016

SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU SENETI MKOA WA DAR ES SALAAM LAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUTOKA KWA


SHIRIKISHO VYUO VYA ELIMU YA JUU SENETI MKOA WA DAR ES SALAAM 

Tunapenda kumpongeza sana Mh Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa hatua mbali mbali za kusimamia ukusanyaji wa mapato, nidhamu ya matumizi, uwajibikaji, kupambana na rushwa, ufujaji wa mali za umma na kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za Taifa Kwa manufaa ya wananchi wote hususani wanyonge. 

Ameendelea kuwathibitishia watanzania Walio wengi kuwa kuteuliwa kwake ndani ya Chama Cha Mapinduzi haikuwa makosa bali alikuwa Chaguo sahihi Kwa wakati na nyakati sahihi Kwa sasa. 

Tunapenda kumuhakikishia wanashirikisho kutoka vyuo vya elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam takribani 32 tunaunga mkono hatua hizi zenye nia na dhamira ya kuhakikisha watanzania wanapata Maendeleo zaidi na Kero kupungua au kumalizika kabisa huku upatikanaji wa huduma muhimu ukiwa rahisi na Kwa ubora. Kasi hii inatufanya wanaCCM vyuoni kutembea kifua mbele kwani utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 utakuwa na hakika zaidi hivyo Nchi yetu kufikia malengo ya kuwa Nchi ya Viwanda. 

Tunaamini kasi hii ya serikali yake itazidi kuongezeka. 

Vile vile tunapenda kumpongeza Kwa uteuzi makini wa wakuu wa mikoa ambao wataimudu kasi ya awamu ya tano ya #HapaKaziTu. 

Tunachukua fursa hii kuwapongeza wakuu wa mikoa waliokuwa katika awamu ya nne na wamebaki katika awamu ya tano hususani mkuu wetu wa Mkoa Ndg Saidi Meck Sadick aliyefanya Kazi na sisi Kwa ushirikiano na ukaribu mkubwa wakazidi kuchapa kazi ili utekelezaji wa ilani ya CCM 2015-2020 ufanikiwe. Pia tunawapongeza sana wakuu wa Wilaya waliopandishwa kuwa wakuu wa mikoa tunaimani nao na hii inadhihirisha chanda Chema huvishwa pete. 

Hapa tunampongeza sana mkuu Wetu wa mkoa mteule wa Dar es Salaam Ndg Paul Christian Makonda. Hakika anastahili, tunamuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake ili kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM. Kwa Wale walioteuliwa Kwa mara ya kwanza tunawapongeza pia na kuwaomba wasimuangushe Mh Rais Magufuli. 
Pia kwa teuzi mbali mbali mbali ambazo Mh.Rais amedhihirisha wazi kuwa ana Imani na vijana wa kitanzania na serikali yake inawaamini vijana. Wito wetu kwa vijana wenzetu wafanye kazi kwa bidii ili waendelee kuilinda Imani ya Mh.Rais kwa vijana.

Kwa niaba ya wanashirikisho wa mkoa wa Dar es Salaam tunamuhakikishia Mh Rais Dkt Magufuli kuwa tutashughulika na yeyote atakayejaribu kupanga kuihujumu au kuikwamisha serikali yako katika utekelezaji wa majukumu yake hususani ya kupambana na ukwepaji kodi, ubadhirifu na usimamizi wa uwajibikaji Kwa nguvu zetu zote. 

Tutazidi kumuombea Mh Rais Dkt Magufuli na tunawaomba watanzania tuzidi kumuunga mkono. 

Imetolewa na 
Imani Moshi Matabula 
Mwenyekiti wa shirikisho vyuo vya elimu ya juu Seneti mkoa wa Dar es Salaam

No comments: