Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel,
Bi. Beatrice Singano Mallya (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi
milioni 11 katibu wa mfuko wa mawasiliano kwa watu Justina Mashiba kwa ajili ya
mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu. yaliyoandaliwa na UCAF (
Universal Communications Services Access Funds ) na kushirikisha wasichana 240
hapa nchini, na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia
mwishoni mwa mwezi huu, Airtel ni mdhamini wa mashindano hayo. Hafla hiyo ya
makabidhiano ilifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar
Es Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
·
Wasichana sita kwenda kushiriki mashindano ya ICT nchini Ethiopia
DAR ES SALAAM
Airtel yakabidi hundi ya
shilingi millioni 11 kwa mfuko wa mawasiliano kwa watu (UCAF) kama wadhamini wa
mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu, yaliyoandaliwa na UCAF
(Universal Communications Services Access Funds ) na kushirikisha wasichana 240
hapa nchini, na kupata washindi sita mwanzoni mwa mwezi huu na kutarajiwa
kuondoka kuelekea nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu na
kushiriki mashindano ya mwisho.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice
Singano Mallya alisema “kama sehemu ya kusaidia jamii ambayo tunafanya
biashara, Airtel Tanzania imeendeleza dhamira yake ya kusaidia
vijana hapa nchini kwa njia mbali mbali. Udhamini huu utawasaidia mabinti hawa
katika safari yao kuelekea nchini Ethiopia katika ngazi nyingine ya juu ya
mashindano haya.
Mallya aliendelea kusema
kuwa kuwainua vijana hawa ni sawa na kuinua taifa letu la kesho. Kwani ujuzi
waliokuwa nao si mdogo hivyo inatupa faraja kubwa hasa sisi wamama kuona kwamba
wamama wa taifa la kesho nao wapo mstari wa mbele katika taaluma ya ICT”.
Akipokea hundi hiyo nae
katibu wa mfuko wa mawasiliano kwa watu, Justina Mashiba alisema "
Tunaishukuru kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kutuwezesha kufanikisha
mashindano haya na vile vile kuwawezesha vijana hawa kuweza kufikia ndoto
zao.Hii inaonyesha dhamira ya dhati ya Airtel ya kuinua vijana hapa nchini na
kuwawezesha kufikia ndoto zao”.
Airtel imejipanga
katika kuinua vijana hapa nchini katika sekta mbali mbali kuhakikisha
kwamba vijana wanainuliwa na kuweza kuendesha maisha yenye matumaini na faraja
tele. Ni makusudio yetu kuendeleza jitihada hizi za kuhamasisha mazingira ya
ICT hapa Tanzania. Aliongeza, “Tunaamini katika uwezo wa ICT kuwawezesha
vijana kutimiza malengo yao muhimu maishani. Sekta ya ICT inajenga fursa
nyingi za ajira kwa vijana ambao wanatamani kutumia vipaji na ujuzi wao
ili kuleta mabadiliko chanya katika maisha yao.”
Na vile vile natoa pongezi za
dhati kwa vijana waioweza kungia katika sita bora na kuweza kwenda
kutuwakilisha nchini Ethiopia. Kwa hivi tulivyoviona tunamatumaini makubwa sana
kwao na tunaamini watatuwakilisha vizuri katika mashindano hayo, aliongezea
Mashiba.
Airtel kupitia huduma zake za jamii, imeweza
kuwafikia vijana zaidi ya 3600 kwa mwaka huu kwa kuwapatia vitendea kazi na
mafunzo mbali mbali ya biashara kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ,ambapo
lengo ni kuwafikia vijana wengi zaidi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment