Tangazo

April 20, 2016

Vijana zaidi ya 300 jijini Dar wanufaika na mafunzo ya ujasiriamali ya Airtel Fursa

Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi Urafiki jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana watatu kati ya 300 waliohudhuria walichaguliwa na kuwezeshwa vitendea kazi kutokana na biashara wanazozifanya.
Mkufunzi kutoka Mpango wa Anzisha na Boresha Biashara yako (SIYB) ulio chini Shirika la Kazi Duniani (ILO), Fidelis Madaha akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi Urafiki jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana watatu kati ya 300 waliohudhuria walichaguliwa na kuwezeshwa vitendea kazi kutokana na biashara wanazozifanya.
Msanii Mrisho Mpoto (kulia), akitoa mada wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, yaliyofanyika kwenye Ukumbi Urafiki jijini Dar es Salaam jana, ambapo vijana watatu kati ya 300 waliohudhuria walichaguliwa na kuwezeshwa vitendea kazi kutokana na biashara wanazozifanya. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.
XXXXXXXXXXXXXXXXXX

  • Vijana Watatu wamewezeshwa vitendea kazi katika warsha ya mafunzo ya ujasiriamali ya Airtel Fursa

Katika jitihada za kusaidia maendeleo, kuinua ujuzi na kujenga ajira katika Jamii ya kitanzania, Airtel Tanzania imeandaa warsha nyingine ya mafunzo ya ujasiriamali kwa zaidi ya vijana 300 na kuwapatia ujuzi muhimu katika kibiashara ili waweza kujiajiri na kuendesha maisha yao ya kila siku.

Warsha hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Urafiki Social Hall, Shekilango jijini Dar es Salaam.

Katika warsha hiyo, kijana Stephano Gimase ambaye alikuwa ni miongoni mwa vijana aliyeweza kushiriki na kuelezea biashara yake ya ufugaji wa kuku mbele ya jopo la washauri na washiriki wengine wa warsha hiyo alibahatika kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya biashara yake pamoja na  kubadilisha maisha yake baada ya mchujo mkali katika warsha hiyo.

Vijana wengine waliohudhuria walionyesha shukrani kwa kampuni ya simu ya Airtel na kuahidi kutumia ujuzi waliopata katika warsha hiyo kwa manufaa yao wenyewe.

"Airtel imetambua changamoto ambazo vijana tunakumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku. Sisi vijana tupo tayari kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu lakini hatuna ujuzi muhimu na zana ili kujenga biashara zetu. Airtel imeliona tatizo hili na kuchukua jukumu hili na kutusaidia sisi vijana, aliongea Yvonne Obeth mmoja wa vijana waliohudhuria.

"Leo hii tumepata stadi za msingi za ujasiriamali, nimejifunza umuhimu wa kutunza kumbukumbu bila kujali udogo wa biashara yangu. Sasa hivi ninajua jinsi ya kuweka vitabu yangu vya akaunti, jinsi ya kutafuta soko la bidhaa zangu hasa kwa kutumia teknolojia ili niweze kufikia wateja zaidi.

Kwa kifupi, warsha hii imekuwa mwangaza wa mafanikio wa maisha yangu. "aliongeza Obeth

Meneja kwa huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema " Hii ni sehemu ya kurudisha fadhila zetu kwa jamii kwa kuunda fursa na kutengeza ajira kwa vijana. Kwani kijana akiwa na ujuzi wa mambo mbali mbali ni faida kwake na ananafasi kubwa ya kutengeneza ajira yake na Jamii inayomzunguka. Tunahitaji kuwawezesha vijana na kubadili mawazo yao kutoka kutaka kuajiriwa  na kujiajiri wao wenyewe.

Kwa upande wake  Stephano Gimase  ambaye ni miongoni mwa vijana watatu walioweza kuwezeshwa na Airtel Fursa katika warsha hiyo na kupatiwa vitendea kazi, aliwashukuru Airtel kwa kuboresha biashara yake “ nimefurahi kupata Fursa hii kubwa ya kupatia vifaa na vitengea kazi, kwangu mimi huu ni muujiza, nimekuja kupata mafunzo lakini nimebahatika kuzaadiwa msaada mkubwa kwaajili ya kuinua biashara yangu. Nawashukuru sana Airtel kwa kuendelea kuwafikia vijana wengi ikiwa ni pamoja na mimi leo.

"Hadi sasa Airtel Fursa imeweza kufikia vijana zaidi  ya 3,600  hapa nchini kupitia mafunzo haya ya elimu ya ujasiriamali.

No comments: