Wakili
maarufu wa Chumi Bw Asheri Utamwa (kushoto ) akizungumza na wanahabari
baada ya mteja wake Chumi kulia kushinda kesi ya uchaguzi.
|
Na fredy mgunda,iringa
CHAMA cha
mapinduzi (CCM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimempongeza
mbunge wa jimbo la Mafinga Bw Cosato
Chumi baada ya kushinda kesi yake
ya uchaguzi dhidi ya aliyekuwa mgombea ubunge jimbo
hilo kupitia chama
cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Bw Willy Mungai .
Akizungumza na wanahabari leo nje
ya viwanja wa mahakama
kuu kanda ya Iringa baada ya
mahakama kutoa huhukumu iliyompa ushindi Bw Chumi ,katibu
wa CCM wilaya ya Mufindi Bw
Jimson Mhagama alisema kuwa baada ya hukumu hiyo ya mahakma kumpa haki mbunge huyo wa CCM kazi
kubwa iliyobaki kwa sasa ni kuona utekelezaji wa ilani ya CCM
unafanywa kwa nguvu zote.
“Hapa kwa hukumu
hii haki imeweza kutendeka
kwani kabla ya kutoa
hukumu jaji alisoma na kutolea
ufafanuzi wa vipengele
vyote ambavyo mlalamikaji
alikuwa anavilalamikia na baada
ya hapo
ndipo alipoweza kutoa hukumu ya kesi hiyo “
Hata hivyo alisema pamoja na hukumu
hiyo kutolewa bado wanachama wa
Chadema na wale wa CCM katika
jimbo la Mafinga hawana budi
kuendelea kuwa wamoja
ili kushikamana na mbunge wao kuleta
maendeleo jimboni .
Kwani alisema
suala hilo la kesi mahakamani mbali ya
kuchelewesha majukumu ya mbunge kwa
wananchi wake bungeni
bado lilikuwa likimfanya mbunge muda wote
kuwa ni mtu wa kuwaza kesi badala ya
kuwaza namna gani ya
kuwatumikia wananchi wake.
“ Ninawaomba
wenzetu Chadema wasifikilie
kukata rufaa kuendelea na
kesi hiyo kwani katika hoja zao
zilizopelekea kwenda mahakamani ufafanuzi
umetolewa vizuri na jaji hivyo
kuendelea kukata rufaa ni
kuendelea kuwacheleweshea wananchi
wa jimbo la Mafinga kupata maendeleo “
Pia alimtaka mbunge
huyo Bw Chumi kufidia
muda ambao ameupoteza kwa kushinda mahakama kusaka
haki kwa kwenda kuwatumikia
wananchi wake kwa kasi ya hapa
kazi tu ili jimbo
hilo lizidi kusonga mbele kwa
maendeleo.
Kwa upande wake Mbunge
Chumi alisema anapenda kuwashukuru
wananchi wake wa jimbo la
Mafinga ambao walitoa
ushirikiano kwa kufika mahakamani
kutoa ushahidi muda
wote na kuwa zaidi anamshukuru
mwenyezi Mungu kwa kusimamia haki katika kesi hiyo .
|
No comments:
Post a Comment