NA K-VIS
MEDIA/Khalfan Said
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na
kampeni yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana
na kazi safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha
Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.
Mafunzo
hayo yaliyofunguliwa leo Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, huko jijini Arusha, ni
muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa wiki mbili zilizopita
jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro,
Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria.
WCF
imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu
uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.
No comments:
Post a Comment